Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, October 9, 2016

Aliyetaka mwamunyange apindue nchi ashinda kesi.soma zaid


MWANAFUNZI wa mwaka wa tatu wa Chuo cha
Maendeleo ya Jamii (CDTI) cha mkoani Arusha,
Allan Mbando, ameibwaga Serikali katika kesi ya
kudaiwa kusambaza ujumbe kupitia Mtandao wa
Facebook akimtaka Mwamunyange apindue nchi.
Katika mtandao huo wa kijamii, Mbando,
anadaiwa kutuma ujumbe uliosomeka kwamba:
“Mwamunyange pindua nchi haiwezekani wote
wawe nje, halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya
kukalia kile kiti.”
Kutokana na madai hayo, Jeshi la Polisi mkoani
hapa lilimfungulia mashtaka Mbando ya kudaiwa
kusambaza ujumbe huo uliokusudia kueneza na
kufanya uchochezi.
Akisoma hukumu ya kesi hiyo mjini hapa juzi,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Arusha, Augustine
Rwizile, alisema mahakama hiyo imepitia kwa
kina hoja na ushahidi wa pande zote mbili katika
kesi hiyo.
Hakimu Rwizile alisema baada ya kupitia ushahidi
katika kesi hiyo, mahakama imejiridhisha kuwa
upande wa Jamhuri katika kesi hiyo haukuweza
kuwasilisha ushahidi unaoweza kumtia hatiani
mshtakiwa.
Alisema mbali na ushahidi huo kutojitosheleza,
pia hapakuwapo na jambo lolote lenye nia ovu ya
kusababisha au kufanya uchochezi katika ujumbe
uliosambazwa na mshtakiwa.
“Sasa mahakama hii inamwachia huru mshtakiwa
baada ya upande wa Jamhuri kushindwa
kuthibitisha mashtaka yake pasipo kuacha shaka
yoyote.
“Lakini pia kama kutakuwa na upande ambao
haujaridhika katika hukumu hii unaweza kukata
rufaa,” alisema Rwizile.
Akisoma hukumu hiyo, alisema ujumbe
uliosambazwa haukuwa na umuhimu wowote kwa
kuwa haukumwelezea Mwamunyange ni nani
katika nchi anayotakiwa kuipindua huku pia
ujumbe huo ukiwa haukutaja nchi iliyolengwa
kupinduliwa.
“Ujumbe ulioandikwa katika Facebook
haumtambulishi Mwamunyange ni nani. Lakini
ujumbe hauonyeshi jambo la msingi lenye
uhusiano wa kisiasa katika Taifa linalodaiwa,”
alisema Rwizile.
Kutokana na sababu hizo ikiwamo ushahidi
uliowasilishwa mahakamani hapo kushindwa
kuthibitisha ujumbe uliosambazwa na mshtakiwa,
mahakama ililazimika kumwachia mshtakiwa.
Mshtakiwa huyo katika kesi hiyo alikuwa
akitetewa na Wakili Moses Mahuna.
Mbando anaongeza idadi ya watu walioshtakiwa
mahakamani kutokana na makosa ya mtandaoni
baada ya Aprili, mwaka huu mkazi mwingine wa
Arusha, Isack Habakuki (40), kufikishwa
mahakamani na kusomewa mashtaka ya
kusambaza lugha ya matusi na dhihaka kwa Rais
Dk. John Magufuli. Baada ya kesi hiyo kuendelea
kusomwa mahakamani hapo, Isack alihukumiwa
kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya
Sh milioni saba na yeye alikubali kuzilipa kwa
awamu.
Mtu mwingine aliyeshtakiwa Aprili, mwaka huu
kwa makosa ya mtandaoni ni kondakta wa
daladala, Hamimu Seif (42), aliyepandishwa
kizimbani kwa kosa analodaiwa kulifanya Machi
10, mwaka huu alipotishia kumuua Rais Magufuli
kwa maneno akiwa katika Baa ya Soweto iliyopo
Makumbusho, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.chanzo mtanzania digi5l

0 comments :

Post a Comment

Back To Top