Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, October 5, 2016

Haya ndio maamzi yaliyochukuliwa dhidi ya Refa aliyechezesha mechi kati ya Simba na Yanga.soma zaid

Katika soka la bongo kwa sasa habari
inayosambaa kwa kiasi kikubwa mtandaoni ni
kuhusiana na muamuzi wa kati aliyechezesha
mechi ya Yanga na Simba October 1 2016 na line
one Samwel Mpenzu kufungiwa miaka miwili,
bado TFF hajatangaza rasmi adhabu hiyo lakini
taarifa zilizoenea mitandaoni ni hizo na TFF
hawajakanusha.
Kuna habari kuwa muamzi Martin Saanya na
msaidizi wake Samuel Mpenzu wamefungiwa
miaka miwili kuchezesha soka, lakini pia
inaripotiwa kuwa kadi nyekundu aliooneshwa
nahodha wa Simba Jonas Mkude imefutwa, hata
hivyo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli ya
1-1.
Maamuzi hayo yanatajwa kufikiwa baada ya
kamati ya saa 72 kukaa na kupitia malalamiko
kuhusu refa kulikubali goli la mkono la Amissi
Tambwe na line one Samwel Mpenzu kulikataa
goli la Ibrahim Ajib kwa kusema kuwa aliotea.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top