Tundu Lissu ashindwa kufika mahamakani kujibu mashitaka ya uchochozi.soma zaid
Mbunge wa Singida Mashariki, jana
alishindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu ili kujibu mashitaka ya uchochezi
huku mdhamini wake akiieleza mahakama kuwa,
yupo jijini Mwanza akisimamia kesi ya Esther
Bulaya, Mbunge wa Bunda katika Mahakama Kuu
ya Mwanza.
Lissu ambaye pia ni wakili wa Mahakama Kuu na
mwansheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo anashitakiwa kwa uchochezi pamoja
na washitakiwa wengine ambao ni ni Jabir
Idrissa, mwandishi mwandamizi wa Gazeti la
MAWIO, Simon Mkina, mhariri wa Gazeti hilo na
Ismail Mehboob, meneja wa kampuni ya
uchapishaji magazeti ya Flint.
Mdhamini wa Lissu, Ibrahim Hemed, alitoa taarifa
ya kutofika kwa mdhamana wake mahakamani
hapo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas
Simba.
Ibrahim alidai kwamba Lissu amempatia taarifa
kuwa ameshindwa kufika kwa sababu yupo
kwenye kesi ya uchaguzi huku Peter Kibatala
wakili wa utetezi akiiomba mahakama ipokee
taarifa za Lissu na ikubali kuhairisha kesi hiyo.
“Lissu ni wakili pekee wa mlalamikiwa Esther
Bulaya katika kesi ya uchaguzi,” alisema Kibatala.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu
Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 31
mwaka huu.
Katika kesi hiyo Lissu anaunganishwa kama
mshitakiwa kufuatia kunukuliwa akitoa maoni
yake katika habari iliyochapishwa na gazeti la
MAWIO ikiwa na kichwa cha habari “Machafuko
yaja Zanzibar.”
POLICE AFANYA.chanzo jungukuu blog
0 comments :
Post a Comment