Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, October 5, 2016

Msajli wa vyama vya Siasa awageukia wadau wa Habari na kutoa onyo kali.soma zaid


Wakati Msajili wa Vyama vya Siasa nchini akitoa
onyo na kuwataka wale wote wanaotumia vibaya
jina la ofisi ya Msajili ili kuichafua ofisi yake au
kwa lengo la kukidhi hisia na matakwa yao
binafsi waache kabisa tabia hiyo, Baraza la
Udhamini la Chama cha Wananchi (CUF)
limesema linafanya utaratibu wa kuzikutanisha
pande mbili za uongozi wa chama hicho kwa
lengo la kumaliza mgogoro uliopo.
“Tunauomba umma wa Watanzania kutambua
kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni
taasisi inayoendeshwa kwa kufuata misingi na
taratibu za sheria za nchi. Aidha tunawaasa
wadau wa habari kutoa taarifa baada ya
kujiridhisha na usahihi wa taarifa hizo, na kujikita
kwenye taarifa zinatolewa rasmi na Ofisi ya
Msajili wa vyama vya Siasa badala ya
kuuaminisha umma na kuupotosha kwa
makusudi,” ilieleza taarifa ya Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Monica Laurent wa
Ofisi ya Msajili.
Kwa siku kadhaa sasa CUF imekumbwa na
mgogoro wa kiuongozi kati ya Katibu Mkuu wa
chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad na
Mwenyekiti wake aliyepata kujiuzulu na kurejea
tena Profesa Ibrahim Lipumba.
Kwa upande wake, Baraza la Udhamini la CUF
kupitia kwa Mwenyekiti wa kikao kilichoketi wiki
hii na Mjumbe wa baraza hilo, Peter Malebo
alisema mgogoro uliopo ndani ya chama hicho
utamalizwa ndani ya chama hicho baada ya
kuzikutanisha pande hizo mbili.
“Tatizo lililopo ndani la CUF ni tatizo la muda
mrefu na wajumbe wa bodi ya chama hicho ndio
wenye jukumu la kumaliza mgogoro huo, lakini
mbaya zaidi baadi ya wajumbe wamekuwa ndio
wanachonganisha na kukuza mgogoro huo badala
ya kuumaliza,” alisema Malebo.
Aidha, Malebo alisema wanampongeza Msajili wa
Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kwa
kutolea ufafanuzi wa sakata la uongozi wa
chama hicho na kumthibitisha Profesa Lipumba
kuwa ni Mwenyekiti halali wa chama hicho kwa
mujibu wa chama chao.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top