Haya ni mambo ya msingi ya kufahamu kabla hujaacha kazi ya kuajiriwa.soma zaid
Leo hii karibu kila mtu aliyeajiriwa ukimuuliza je,
unafurahia maisha ya kuajiriwa? Atakwambia
hapana ila natamani kujiajiri, na endapo
utaendelea kumuuliza ni kwa nini unatamani
kujiajiri? Utamsikia anasema nataka kuwa huru
na muda na pia nahitaji uhuru wa kipesa.
Majibu hayo kwa mtazamo wa wengi ni sawa,
ila kuna kitu ambacho ni vyema ukakijua kabla
ya kuamua kuacha kazi na kwenda kujiajiri.
Kujiajiri kuna hitaji ujasiri wa hali ya juu sana
maana kuna changamoto zaidi ya kuajiriwa.
Hivyo nakusihi ufikirie kwa umakini sana suala
zima la kuacha kazi kabla kwenda kujiajiri.
Na endapo utaamua kuacha kazi ya kuajiriwa
bila ya kufikiria ipo siku utakuja kujutia uamuzi
wako. Hivyo ni vyema ukafikiria mara mbili
kabla ya kufanya maamuzi magumu.
Mambo ya msingi ya kuzingatia kabla ya
kuacha kazi.
1. Kuwa na nidhamu ya muda.
Kwa kuwa kwa sasa bado umeajiriwa, hivyo
huna jukumu la kufanya maamuzi ya matumizi
ya muda, Bali unafanya kazi kutokana na muda
ambao muajiri wako ameamua yeye kukupangia
kuweza kufanya kazi.
Na kwa kuwa umezoea kufanya kazi kutokana
na amri ya mwajiri wako, hata pale ambapo
utaamua kuacha kazi fahamu fika ya kwamba
suala la kuwa na nidhamu ya muda kwako ni
suala gumu, hivyo unatakiwa kufanya jitihada
zako binafsi kadri iwezekanavyo hasa katika
matumizi sahihi ya kufanya kazi hasa suala
zima la uzalishaji wa mali au huduma.
Nazungumza suala zima la matumizi ya muda
kwani hapa ndipo ambapo tunapata makundi
mawili ya watu waliofanikiwa na wasiofanikiwa.
Hivyo ni jambo jema kuhakikisha unazingatia
matumizi sahihi ya muda ili pindi utakapoacha
kazi wewe ndiye ambaye utakuwa na jukumu la
kupanga muda wa kufanya kazi na ni muda gani
utakuwa ni wa kupumzika. Pia ikiwezekana
ongeza matumizi sahihi ya muda mara mbili
zaidi ya ulivyokuwa umeajiriwa.
2. Kutokuahirisha kufanya mambo ya msingi.
Utakuwa shahidi ya kwamba wakati umeajiriwa
suala zima la uahirishaji wa kufanya mambo ya
msingi lilikuwa ni suala gumu sana labda awe
ameamua mwajiri wako. Kama ndivyo hivyo
basi pale ambapo utakuwa umeamua
mwenyewe kuacha kazi na kuamua kufanya
kazi mwenyewe hivyo huna budi kuhakikisha ya
kwamba suala zima la uhairishaji mambo
linakuwa ni suala ambalo halina nafasi katika
maisha yako.
Ukiwa ni mtu wa kufanya kazi kwa kuamua
kutenda bila kuahiirisha vitu vya msingi ama
hakika utafika kilele cha mafanikio yako ndani
ya muda mfupi. Ni vyema kulizingatia hili, kwani
hili ndilo ambalo limewafanya watu wengi
ambao waliacha kazi kuwa na maisha duni
zaidi, kwani wengi wao walikuwa ni waahirishaji
wazuri wa vitu vya msingi.
0 comments :
Post a Comment