Meya wa Manispaa ya Sumbawanga ashikililiwa na Polisi kwa tuhuma ya kuhusika kuketeza misitu kwa Moto.soma zaid
Polisi mkoani Rukwa inamshikilia Meya
wa Manispaa ya Sumbawanga, Justine
Maliwasa (CCM) akituhumiwa kuhusika na
kuteketezwa kwa moto msitu wa hifadhi
wa Mbizi na kusababishia serikali hasara
ya zaidi ya Sh milioni 226.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa,
George Kyando amethibitishwa kuwa
mwanasiasa huyo alikamatwa juzi na
kuhojiwa kwa saa kadhaa.
“Kweli (Maliwasa) amehojiwa lakini ni
mahojiano tu yanayoendelea, taarifa zaidi
itatolewa hadharani baadaye kwa sasa
bado anahojiwa.
“Anahojiwa baada ya watuhumiwa
tuliowakamata kwa kosa la kuteketeza
msitu huo wa hifadhi kwa moto walipodai
kuwa wametumwa na Meya huyo
(Maliwasa),“ alisisitiza.
Taarifa kutoka ndani ya jeshi hilo
zinaeleza kuwa mwanasiasa huyo ambaye
ni Diwani wa Kata ya Senga katika
Manispaa ya Sumbawanga, alihojiwa
katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini hapa
kuanzia saa tano asubuhi hadi usiku.
Msitu huo ni chanzo kikubwa cha maji
cha wakazi wa mji wa Sumbawanga na
vitongoji vyake kwa asilimia 80.
Msitu huo wenye ukubwa wa ekari 1,260
ambao umepandwa miche ya miti mwaka
2014, unasimamiwa na Mamlaka ya
Huduma za Misitu (TFS).
Chanzo: Fahari News
0 comments :
Post a Comment