Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, October 29, 2016

Chama cha ACT Wazalendo kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya kiongozi wake zitto Kabwe.soma zaid

Chama cha ACT-Wazalendo kimesema
kimeshtushwa na tuhuma dhidi ya
kiongozi wake wa chama, Zitto Kabwe
kwamba ana miliki mali za kifisadi pamoja
na kuhusishwa na ununuzi wa ardhi
maeneo ya Kigamboni uliofanywa na NSSF
kwa bei ya milioni 800 kwa ekari moja,
wakati bei halisi ni milioni 25 na kwamba
kitendo hicho kimeitia hasara serikali .
Tuhuma hizo zilitolewa jana na Msemaji
wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Christopher Ole Sendeka, ambapo
alivitaka vyombo vya uchunguzi kufanya
uchunguzi katika shirika hilo ili kubaini
waliohusika kwa ajili ya kuchukuliwa
hatua za kisheria, huku akimhusisha Zitto
katika uchunguzi huo.
Ole Sendeka alitaka akaunti za benki za
Zitto pamoja na maisha yake binafsi
kuchunguzwa kama yana uhalisia na
kipato chake halali.
Tuhuma hizo zimekiibua chama cha ACT,
ambapo leo Katibu wa Bunge na Serikali
za Mitaa ACT, Habibu Mchange amevitaka
vyombo vya uchunguzi haraka
iwezekanavyo kuchunguza mali, madeni,
akaunti zote za benki pamoja na mfumo
wa maisha ya Zitto.
“ACT imeshtushwa na tuhuma, kashfa,
porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa
jana na Ole sendeka dhidi ya kiongozi wa
chama chetu,” amesema.
Amesema kuwa, katiba ya chama hicho
huwataka viongozi wote kuweka
hadharani matamko ya mali zao na
madeni na kwamba Zitto alitekeleza
matakwa hayo ya kisheria hivyo mali na
madeni yake yako hadharani na
mtandaoni.
“Tunaamini kama kuna kiongozi ambaye
mali, madeni, maslahi, na akaunti zake
viko wazi basi ni ndugu Zitto,” amesema.
Aidha, Mchange amedai kuwa,
kilichomsukuma Sendeka kutoa tuhuma
hizo kwa Zitto ni harakati zake za
kuupinga muswada mpya wa habari.
“Tuhuma za olesendeka kuna kitu nyuma
yake, jitihada za zito za kupambana na
mswada wa habari ndizo zilizomuibua,
sababu wanataka upitishwe ili kuviua
vyombo vya habari,” amesema.
Amesema ACT itaendelea kuisimamia
serikali katika mambo ya bungeni kama
anavyofanya mbunge na kiongozi wao wa
chama.
Chanzo: Dewji Blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top