Breaking News
Loading...

Advert

Friday, October 7, 2016

Mtu mmoja amefariki dunia kwa kuilpigwa risasi wakati walipokuwa akijaza fomu ya mkopo.soma zaid

WATU wasiofahamika wamevamia kwenye ofisi
ya serikali ya kijiji cha Kimanzichana Kusini,
Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani na
kumfyatulia risasi kichwani, Bakari Said (45) na
kusababisha kupoteza maisha wakati akijaza
fomu kwa ajili ya kuchukua mkopo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa huo,
Boniventura Mushongi, tukio hilo lilitokea juzi
saa 5:00 asubuhi baada ya Said kufika katika
ofisi ya mtendaji wa kijiji na kujaza fomu za
mkopo kutoka Benki ya Akiba (ACB).
"Akiwa anajaza fomu yake ya mkopo, walitokea
watu wawili wakiwa na silaha mbili na kuanza
kuwafyatulia risasi na kutoweka kusikojulikana
wakitumia usafiri wa pikipiki," alisema.
Alisema mbali na kufanyika kwa mauaji hayo, pia
walimjeruhi kwa kumpiga risasi kwenye mkono
wa kushoto Omary Ally (55), ambaye ni Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Kimanzichana Kusini.
Kamanda Mushongi alisema ofisa mtendaji wa
kijiji huyo amelazwa kwenye Hospitali ya Wilaya
ya Mkuranga kwa matibabu.
Aliongeza kuwa polisi walikuta maganda mawili
ya risasi kwenye eneo la tukio yaliyotumika
katika silaha ya Semi-Automatic Rifle (SAR)
ama Sub Machine Gun (SMG).
Kamanda Mushongi alisema Jeshi la Polisi Mkoa
wa Pwani litahakikisha linapambana kwa nguvu
zake dhidi ya watu wenye nia ya kuwatia hofu
wananchi.
KUUNGUA KWA BWENI
Katika tukio lingine, Kamanda Mushongi alisema
moto uliozuka juzi kwenye bweni la wasichana
wa Shule ya Sekondari Moreto iliyopo Kata ya
Lugoba Tarafa ya Msoga wilayani Bagamoyo,
uliteketeza mali zote za wanafunzi ambao
walikuwa darasani.
Alifafanua kuwa moto huo ulianza saa 4:45
asubuhi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa shule hiyo, Justine
Lyamuya, walianza kuona moshi mzito katika
moja ya bweni linalotumiwa na wasichana na
walipofuatilia, walikuta moto tayari umeshashika
kwenye bweni hilo huku jitihada za kuuzima
zikishindikana.
Kamanda Mushongi alisema Jeshi la Polisi Mkoa
wa Pwani linafanya uchunguzi wa tukio hilo
kubaini chanzo chake kwa kuwa shule hiyo
inatumia nishati ya umeme wa jua.
Source: Nipashe

0 comments :

Post a Comment

Back To Top