Sumaye apata taarifa kutaka kuodolewa anapoishi.soma zaid
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya
Tatu, Frederick Sumaye amesema kuwa baada
ya kutangazwa mchakato wa kunyang’anywa
shamba lake la Mwabwepande, amepata taarifa
ya kutaka kuondolewa anapoishi pia.
Sumaye ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache
baada ya Waziri Wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza
kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa
kumnyang’anya mwanasiasa huyo shamba la
Mwabwepande kwa madai ya kutoliendeleza kwa
muda mrefu.
“Hapa ninapoishi naambiwa kuna maelekezo
yametoka juu kuwa sijapaendeleza. Sasa kama
sijapaendeleza mbona ninaishi hapahapa,”
Sumaye amekaririwa na gazeti la Nipashe.
Aidha Sumaye amesema kuwa ingawa alimsikia
Waziri Lukuvi akieleza kuwa tayari wameshampa
notisi ya siku 90 kuhusu kunyang’anywa shamba
lake la Mwambwepande, hadi jana hajaipata
notisi hiyo licha ya kufanya jitihada za kuifuatilia.
Alisema kuwa anashangazwa na uamuzi huo wa
Waziri kwani kesi inayolihusu shamba hilo bado
inaendelea mahakamani kutokana na uvamizi wa
wananchi na kwamba Mahakama imezitaka
pande zote mbili kutofanya chochote kwenye
ardhi hiyo.
Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Chadema alisema kuwa
anachokifahamu ni kwamba alipokea notisi ya
kuondolewa katika shamba lake la Mvomelo kwa
madai ya kushindwa kuliendeleza kwa muda
mrefu.
“Ninachokijua ninaandamwa kisiasa. Shamba
langu la Mvumelo naambiwa sijaliendeleza.
Kwenye hilo shamba niemjenga nyumba ya
kuishi, ghala, kuna trekta na vifaa vingine.
Ninalima mazao na nimefuga zaidi ya ng’ombe
200, nina kondoo 300 na nimechimba visima
viwili vya maji halafu serikali inasema
sijaliendeleza,” alisema Sumaye.
Alisisitiza kuwa ingawa anaamini anaandamwa
kisiasa kwa kunyang’anywa mashamba yake,
hatarejea CCM hata akinyang’anywa mashamba
yote aliyoanayo.
Sumaye alihama CCM mwaka jana, miezi
michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu
na kujiunga na harakati za kumpigia kampeni
mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward
Lowassa. Baada ya uchaguzi huo alitangaza
kujiunga rasmi na Chadema.
0 comments :
Post a Comment