Sakata la UDA limeibuliwa upya na hii ndio hali halisi.soma zaid
Sakata la uuzwaji wa Shirika la Usafiri Dar es
Salaam (UDA) linazidi kuchukua sura mpya
baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
za Mitaa (LAAC) kuitaka serikali kuwasilisha
mkataba wa uuzwaji wa hisa za kampuni ya
Simon Group ndani ya wiki mbili.
Wiki iliyopita kamati hiyo iliutaka uongozi wa Jiji
la Dar es Salaam kueleza namna kampuni ya
Simon Group ilivyoingia na kuwa mmoja wa
wamiliki wakubwa wa hisa za UDA. Maelezo
yaliyotolewa hayakuiridhisha kamati ambapo jana
walirudi tena mbele ya kamati wakiambatana na
Mwansheria Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala la Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
na Msajili wa Hazina ili kueleza ukweli juu ya
sakata hilo na wamiliki halali wa UDA.
Serikali kwa upande wake imekiri mbele ya
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa
(LAAC) kuwa inamiliki hisa nyingi zaidi katika
shirika hilo la usafiri.
Aidha, iliieleza kamati kuwa hisa zote ambazo
hazikuwa zimegawanjwa asilimia 52 za UDA
zilizouzwa kwa kampuni ya Simon Group bila
kufuata taratibu zimerejeshwa serikalini.
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu
wa Serikali (CAG) anaeleza kuwa UDA ina hisa
milioni 15 ambayo kila moja ina thamani ya
shilingia 100.
Asilimia 47.5 ya hisa hizo sawa na hisa milioni
7.1 ziligawanywa katika makundi mbalimbali
ambapo Jiji la Dar es Salaam lilipata hisa
asilimia 51 sawa na hisa milioni 3.6. Makundi
mengine yaliyogawiwa ni serikali iliyokuwa na
jumla ya hisa milioni 3.9 sawa na asilimia 49.
Hivyo hisa milioni 7.8 zilizobaki ambazo ni sawa
na asilimia 52 kuuzwa kinyemela na Bodi ya UDA
kwa kampuni ya Simon Group ambazo ndizo
zilizorejeshwa.
Wanahisa wengine wa kampuni ya Simon Group
ni pamoja na, Robert Simon Kisena (hisa 94,000),
Simon Robert Kisena (hisa 20,000), Gloria Kisena
(hisa 20,000). Wengine ni Kulwa Simon Kisena,
William Kisena, Modesta Pole na Juma Kapuya
kila mmoja akimiliki hisa 10,000, Gilbert Ngalula
(hisa 6,000) na George Simon (hisa 5,000).
Kamati ilihitimisha kwa kuitaka serikali
kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha kuwa
inamiliki hisa nyingi zaidi katika Shirika la Usafiri
la Dar es Salaam (UDA) kama ilivyoeleza.chanzo swahili times
0 comments :
Post a Comment