TANESCO imasaini mkataba na makambuni matatu kujenga njia ya umeme itakayounganisha Tanzania na Kenya.soma zaid
SHIRIKA la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO)
, limesaini mkataba na makampuni matatu
kujenga njia ya umeme, (Transmission lines),
wa Msongo wa Kilovolti 400 utakaounganisha
Tanzania na Kenya.
Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo,
imefanyika leo Oktoba 7, 2016 makao makuu ya
TANESCO jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika
hilo la Umeme linalomilikiwa na serikali,
limetiliana saini mikataba hiyo na makampuni
ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na
Kalpa-Taru.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi
Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye
urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani
Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye
mpaka wa Tanzania na Kenya.
Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo
wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96
kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi
eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya,
(Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya
umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa
upande wa Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi
Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni
ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton
wakisaini mkataba huo.
“Napana niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo
wa miradi mikubwa inayotekelezwa na TANESCO
na utawezesha usafirishaji wa umeme wa
Mgawati 2000 katika pande zote Kenya na
Tanzania”. Alifafanua Mramba.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema,
utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki
ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la
Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa
gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26
utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na
miaka 2.
“Dola za Marekani Milioni 258.82, zitatumika
kujenga upande wa Tanzania na Dola za
Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika kujenga
mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi
Mramba.
Hata hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa onyo
kwa wakandarasi waliopewa kazi hiyo
kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania,
(TANESCO), Felchesmi Mramba, (kushoto),
akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni
ya Bouygues Energies & Service, Patrick Canton
baada ya kusaini, mradi wa ujenzi wa njia ya
umeme (transmission line) itakayounganisha
Tanzania na Kenya, makao makuu ya TANESCO
jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016.
Shirika hilo limeingia mkataba na makampuni
matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa
Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la
Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa
gharama ya dola za Kimarekani 309.26
“Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini
mradi ndani ya muda kama ambavyo
tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa
kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa mkataba ni
kushindwa kufanya kazi na sisi kama TANESCO
hatutakubaliana na hilo.” alionya Mhandisi
Mramba.
Naye Mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia
Kandiero, alitoa hakikisho kuwa benki hiyo
itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii,
kwa manufaa ya eneo lote la Afrika.
Kwa upande wake, Afisa Miradi msaidizi wa
JICA, Apolei Rosina, naye aliungana na AfDB,
kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya
Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza
miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa leo.
0 comments :
Post a Comment