Utumiaji wa mitandao ya intanet unaweza kuwa chanzo cha magongwa mengine ya akili.soma zaid
Uraibu wa mitandao ya intaneti unaweza kuwa
chanzo cha magonjwa mengine ya akili, ripoti
inasema.
Utegemezi wa mitandao hiyo unahusishwa na
sonona, wasiwasi na mfadhaiko hivyo kuathiri
uwezo wa kuwaza na kuamua wa mhusika.
Maendeleo ya teknolojia yameleta mabadiliko
makubwa katika matumizi ya mitandao kutokana
na taarifa za kila aina kupatikana kwa urahisi
zaidi kwa kutumia simu za mkononi au kompyuta
hivyo kurahisisha maisha ya wengi.
Watu hutumia muda mwingi mitandaoni
wakitafuta taarifa, kufanya ununuzi ya bidhaa au
huduma, kucheza michezo tofauti iliyopo,
kutazama video na picha au kutumiana
baruapepe.
Licha ya faida nyingi zilizopo, matumizi ya
mitandao hiyo yakizidi huweza kusababisha
magonjwa au matatizo ya akili mfano sonona,
msongo wa mawazo na wasiwasi.
Katika utafiti uliofanywa na watafiti kutoka nchini
Canada umebaini kuwa matumizi ya mitandao
yaliyopitiliza yanaweza kuwa kisababishi cha
matatizo mbalimbali ya afya ya akili miongoni
mwa wanafunzi hasa wa vyuo vikuu.
Katika tafiti huo watafiti walitathmini matumizi
ya mtandao kwa wanafunzi 254 kutoka Chuo
Kikuu cha McMaster kilichopo Ontario kwa
kuzingatia muda ambao mwanafunzi husika
ameutumia kwenye intaneti na madhara
yanayoweza kujitokeza.
Kwa kutumia kipimo cha kubaini kiasi cha uraibu
wa intaneti au Internet Addiction Test (IAT)
kama wanavyokiita pamoja na vigezo vingine
walivyoviweka walipata matokeo yasiyo na shaka
kuwa matumizi yaliyopitiliza ya intaneti ni chanzo
cha magonjwa ya akili.
Majibu ya utafiti huyo ambayo yaliwsilishwa
kwenye mkutano wa mwaka wa madaktari
bingwa wa magonjwa ya akili (ECNP) uliofanyika
huko Vienna, Austria yalionyesha wengi wa
washiriki hao walikuwa wameathirika.
Majibu yalibainisha wanafunzi 33 walikutwa na
viashiria vya kuathirika na matumizi ya mtandao
na 107 walikutwa na matatizo yatokanayo na
matumizi ya mitandao.
Kiongozi wa jopo hilo, daktari bingwa wa
magonjwa ya akili kutoka chuo kikuu hicho,
Profesa Michael Van Ameringen alisema:
“Matumizi ya mtandao yaneobgezeka sana ndani
ya miaka 18 iliyopita. Watu wanawasiliana kwa
njia ya video, mitandao ya kijamii, kufuatilia
habari na mengi mengine. Matumizi yakizi
husababisha tatizo.”
Utafiti huo umebaini kuwa wengi wa washiriki
walioathirika na matumizi ya intaneti
wanashindwa kudhibiti ratiba zao za kila siku
huku wakiwa na msongo wa mawazo, wavivu na
wasioweza kuzingatia wafanyalo. Walibainika pia
kupangilia mambo yao pamoja na kuratibu muda.
Daktari bingwa wa magonjwa ya akili, Profesa
Jan Buitelaar wa Hospitali ya Nijmegen ya Chuo
Kikuu cha Radboud huko Uholanzi anasema:
“Uraibu wa intaneti ni sehemu ambayo
haijafanyiwa utafiti wa kutosha lakini matumizi
yaliyopitiliza yanaweza kusababisha uraibu.”
Tanzania
Mtaalamu wa afya ya akili, Dk John Chikomo
anasema kuwa ni kweli mtu ambaye ana
utegemezi mkubwa katika mitandao anaweza
kupata matatizo ya akili na kwakuwa mitandao
huweza kuiteka akili ya mtu na kumfanya awe
tegemezi wa mitandao.
Dk Chikomo anaunga mkono matokeo ya utafiti
huo na anatoa mfano wa mtu ambaye amezoea
kunywa pombe inapotokea ameikosa kwa muda
huanza kujisikia kama anaumwa na mwenye
mawazo lakini mara tu anapopata pombe hali
yake huimarika na kuwa mwenye amani.
Hali kadhalika katika mitandao endapo mtu
amejizoesha kuperuzi kwenye mitandao ya
kijamii kama facebook, twiter, whatsApp na
kutazama video hufarijika lakini inapoikosa hali
yake kubadilika ndipo mtu anaweza kupata
sonona, msongo wa mawazo na wasiwasi.
Dalili
Wataalamu wanaeleza kuwa kuna dalili nyingi za
mtu aliathirika na matumizi yaliyopitiliza ya
mitandao ya intaneti. Kujisikia furaha kila
unapotumia kompyuta au simu kama njia pekee
ya kumfariji ni moja ya dalili hizo.
Nyingine ni kushindwa kufuata ratiba ipasavyo
kiasi cha kuweza kuacha mambo ya msingi na
kutumia muda mwingi kuperuzi mitandaoni.
Wakati mwingine hamu ya kufanyakazi hupungua.
Inapotokea hupendi kazi yako kama ilivyokuwa
hapo awali, wataalamu wanaeleza kuwa ni dalili
kuwa intaneti inaaza kukuathiri. Hii inaweza
kwenda sambamba na kujisikia uvivu.
Wengine hawathamini muda. Baadhi ya watumiaji
wanaoathirika hawawezi kuthamini muda wao
kwani huona ni vyema kukaa na kuperuzi
mitandaoni kuliko kufanya mambo ya msingi
kama kusoma au kazi za ofisini.
Kutokuwa mkweli. Kutokana na kupitiwa mtu
huanza kuwa muongo kutokana na kushindwa
kutimiza ahadi.
Hali hii inajidhihirisha hasa kwa vijana ambao
wanaopenda kuangalia video mitandaoni hasa za
ngono kutokana na kutekwa akili.
Athari;
Dk Chikomo anaeleza mazoea haya huweza
kuibua tabia mpya ambazo mtu hakuwanazo
kutoka na taarifa anazokutana nazo mtandaoni.
Kwa wanafunzi anasema wengi wanashindwa
kufaulu masomo yao kwa kiwango cha juu
kutokana na kutegemea intaneti kuwapa majibu
ya kila kitu.
“Ukishakua mlevi wa mitandao ni vigumu kuacha.
Wagonjwa wanahitaji ushauri nasaha kutoka kwa
mtaalamu ili kuwapa njia mbadala,” anasema Dk
Chikomo.
Mwalimu sekondari jijini Dar es Salaam,
Emmanuel Mhando anasema madhara hayo
yanajitokeza kwa wanafunzi wengi sio wa vyuo
vikuu pekee.
“Vijana wengi wanaomiliki siku za kisasa wana
kumba na tatizo hili. Wanafunzi wengi wanatumia
simu zao kutafuta majibu ya maswali na kazi
mbalimbali za darasani. Wanazitegemea zaidi
simu kuliko akili zao,” anasema.
Anaeleza kuwa wapo baadhi ambao hukamatwa
wakizitumia darasani hivyo kulazimika kuwaita
wazazi au walezi wao ili kuwashirikisha juu ya
umiliki wa vifaa hivyo vya mawasiliano.
“Familia zinapaswa kusaidia hili. Vijana
wanatakiwa wasaidiwe ili waweze kufanya
shughuli nyingine wanazotakiwa kuzitekeleza,”
anasema Emmanuel.
Matibabu;
Suala la matibabu kwa mtu ambaye anatatizo la
utegemezi wa mitandao ni jambo amabalo
limetajwa kuwa ni gumu kwa namna yake
kutokana na kwamba mtu anahitaji ushauri
nasaha kutoka kwa wataalamu wa akili ili kumpa
njia mbadala ya kuachana na tabia hizo.
“Ni vigumu kumwambia mtu aachane na
matumizi ya mitandao ikiwa yeye mwenyewe
anaona ni jambo zuri kwake kinachohoitajika ni
ushauri kutoka kwa mtaalamu,” anasema Dk
Chikomo.
Dk Elizabeth Wampembe wa Chuo cha Kikuu cha
Muhimbili (Muhas), anasema matatizo ya kijamii
na kifamilia yanaweza kumfanya mtu kuona hiyo
ndiyo njia pekee ya kujifariji na kuepuka matatizo
yanayomkabili.
“Mtu akiitegemea intaneti huweza kuathirika
kisaikolojia na kubadilika kitabia kwa ujumla hali
inayoweza kumfanya ajihusishe na mambo yasiyo
ya kawaida,” anasema Dk Eliza.
Anasema kutokana na hali ilivyo sasa watu
wenye uwezekano wa matatizo ya akili kutokana
na matumizi ya mitandao ni mkubwa kutokana na
kutumia muda mwingi wakiperuzi mitandaoni
kunakochangiwa na upatikanaji wa intaneti ya
uhakika.chanzo mwananch
0 comments :
Post a Comment