Zari,Hamisa Mubeto hapatoshi ngoma bado mbichi.soma zaid
.
DAR ES SALAAM: Kimenuka tena! Ndiyo
unavyoweza kusema baada ya mzazi mwenza wa
staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
kutupia picha ya hereni kwenye Mtandao wa
Kijamii wa Snapchat huku akitupa dongo kwa
kusema aliyesahau vitu vyake aende akavitoe,
bifu limeibuka upya mitandaoni.
Mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari
The Boss Lady’.
Baada ya kutupia picha ya Snapchat hiyo,
mashabiki mbalimbali wa mtandao huo
walijiongeza na kuoanisha na picha ya
Mwanamitindo Hamisa Mobeto kwa kufananisha
hereni alizovaa siku za nyuma zikifanana na hizo
alizodai Zari zimesahaulika kwenye chumba cha
Diamond, nyumbani kwake, Tegeta-Madale jijini
Dar.
Mbali na mashabiki hao kujiongeza, mjadala
mzito uliibuka pia wakidai ugomvi wa Zari na
Mobeto si rahisi kumalizika maana kati yao
hakuna anayeweza kuwa mpole na kumwachia
mwenzake atambe. “Hili lazima ni dongo kwa
Mobeto, yaani hawa, hauwezi kupita muda
hawajazinguana, kweli mapenzi yanauma lol…”
aliandika mmoja wa mashabiki wanaotumia
mtandao huo wa Snapchat.
Staa wa Bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ akiwa na mpenzi wake Zari .
Mjadala ulikuwa mkubwa huku kila mmoja
akimtetea anayempenda hadi mashabiki hao kufi
kia hatua ya kutukanana mitandaoni. Kuna
ambao walimtetea Zari lakini wengine walikuwa
upande wa Mobeto.
Risasi Jumamosi lilimtafuta mwanamitindo huyo
ili aweze kufungukia hayo madai ambapo alisema
ameziona lakini hakutaka kufunguka kama ni
zake au la: “Nimechukizwa na kitendo hicho.
Kitendo hicho kimenifanya mimi nitukanywe sana
matusi ya nguoni kwenye mitandao ananitafuta
sana Zari lakini ipo siku atanipata,” alisema
Mobeto. Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao
kuingia kwenye bifu ambapo inadaiwa penzi la
Diamond ndilo linalowatia ‘uchizi’ hata kuwafanya
w a k w a r u z a n e k i l a mara
0 comments :
Post a Comment