Breaking News
Loading...

Advert

Monday, October 3, 2016

Wakazi 3 wa kijiji cha mbala mkoani mbeya wahukumiwa kunyongwa.soma zaid

Mbeya. Vielelezo viwili na mashahidi 13 wa
upande wa mashtaka vimeiwezesha Mahakama
Kuu Kanda ya Mbeya, kuwahukumu vifo wakazi
watatu wa Kijiji cha Mbala, Wilaya ya Chunya
mkoani hapa.
Kutokana na ushahidi huo, Mahakama hiyo
iliwahukumu watu hao kunyongwa hadi kufa
baada ya kuwaua kwa makusudi wakazi wenzao
watatu.
Washtakiwa hao ni Apolinari Mateo (30),
Barnaba Siwinga (38) na Michael Claud (24),
ambao kwa pamoja walipatikana na hatia ya
kuwaua Julius Mwamasonga, Sabela Boniface
na Maongezi Mkusi waliokuwa wakiishi kijijini
hapo.
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Dk Adam Mambi
alisema Mahakama imeridhishwa na ushahidi
huo uliotolewa na upande na walalamikaji pasipo
kuacha shaka kuwa, washtakiwa walitenda kosa
hilo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top