Breaking News
Loading...

Advert

Monday, November 7, 2016

Asikali nchini Canada wanachunguza kelele za ajabu kutoka bahari ya Antarct

Kelele hizo ziliripotiwa na watu wa eneo hilo
kwamba zimewatisha wanyama na kuwafanya
wakimbie mbali katika kipindi cha miezi
michache iliyopita.
Jeshi la Canada limechunguza kelele za ajabu
zenye mlio mkali zinazotoka kwenye sakafu ya
bahari katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa
urahisi la kanda ya Arctic, maafisa wameiambia
BBC
Kelele hizo za ajabu ziliripotiwa na watu wa
eneo hilo kwamba zimewatisha wanyama na
kuwafanya wakimbie mbali katika kipindi cha
miezi michache iliyopita.
Ndege ya kijeshi imefanya msako wa aina mbali
mbali wa kunasa sauti hizo, wamesema maafisa
siku ya Ijumaa.
Hata hivyo jeshi hilo la Canada limesema hadi
sasa haliwezi kuelezea sababu ya "sauti hizo za
ajabu".
" Mhudumu wa ndege hiyo amesema
hawakuweza kubaini kitu chochote cha ajabu
kwenye uso wa bahari ama chini ya uso wa
bahari ," imesema taarifa ya jeshi iliyotolewa
kwa BBC.
" Kile ambacho alikiona ni makundi mawili ya
nyangumi na sili wa bahari wenye pembe sita
katika eneo lililochunguzwa''
Msemaji wizara ya usalama wa taifa mjini
Ottawa amesema kuwa sababu ya kelele hizo -
amazo wakazi wanasema zinaweza kusikika
hata kupitia kuta za maboti zimesalia kuwa
vigumu kutambuliwa.
Eneo ambalo llimekumbwa na kelele za ajabu
Sauti hizo ambazo zimekuwa zikisika katika
kipindi chote cha majira ya joto katika maeneo
ya baridi, mbunge Paul Quassa ameiambia CBC,
yapata kilomita 120 kaskazini-magharibi mwa
kijiji kidogo cha Igloolik.
Eneo hilo ni njia ya vijito vya maji katika
Nunavut, eneo ambalo ni makazi mapya ,
makubwa na yenye kukaliwa na idadi ndogo ya
watu nchini Canada, karibu na Greenland.
" Ni moja ya maeneo maarufu zaidi kwa
shughuli za uwindaji nyakati za majira ya joto
na baridi kwasababu ni eneo pana zaidi la maji
lililozingirwa na barafu ambayo ina wanyama
wengi wa baharini ," Amesema Bwana Quassa.
" Na wakati huu, majira haya ya joto, kulikuwa
hakuna mnyama yoyote. Na hili likawa suala la
kushangaza."
Maelezo mbali mbali kuhusu sauti hizo za
kushangaza yamekuwa yakiwasilishwa katika
vyombo vya habari nchini Canada.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top