Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, November 5, 2016

Asasi za kiraia nchini zililazimika kuanzisha mchakato wa kudai katiba mpya.soma zaid

Asasi za Kiraia nchini jana ziliazimia kuanzisha
mchakato wa kudai katika mpya huku zikiahidi
kutowahusisha wanasiasa katika harakati hizo,
tofauti na ilivyokuwa awali.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kumalizika kwa mkutano wao uliofanyika jijini Dar
es Salaam, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa
Haki za Binadamu, Onesmo Ole Nguruma alisema
kuwa wameazimia hayo ili mchakato huo uwe wa
wananchi na sio wa wanasiasa.
“Mwaka jana mchakato ulikuwa wa kisiasa zaidi,
sasa hivi tunataka kuanzisha mchakato
utakaokuwa wa wananchi,” alisema Ole
Nguruma.
Alisema kuwa baadhi ya wanasiasa walichangia
kukwamishwa kwa mchakato huo kwakuwa
baadhi yao mwishoni walijikuta wakitofautiana na
wengine kuzila kuendelea na harakati hizo.
Katika hatua nyingine, Rais John Magufuli jana
aliwaambia wahariri wa vyombo vya habari katika
mahojiano ya ana kwa ana Ikulu jijini Dar es
Salaam, Rais Magufuli alipoulizwa kuhusu
mpango wa kuanzisha upya mchakato wa Katiba
Mpya alisema “niacheni ninyooshe nchi kwanza.”
Rais Magufuli alisema kuwa yeye
hakulizungumzia suala hilo kwenye kampeni zake
zote.
Mchakato wa kupata katiba mpya ulianzishwa na
Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya
Kikwete na kuunda Tume iliyokuwa chini ya
uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba ambaye
alitengeneza rasimu iliyowagawanya wabunge wa
bunge la katiba, wanaharakati pamoja na Serikali.
Wanaharakati wanadai rasimu ya Jaji Warioba
iliyowasilishwa kwenye Bunge la Katiba na
mapendekezo ya wananchi ndiyo ipewe
kipaumbele, huku Serikali ikiwa imebadili baadhi
ya maeneo hali iliyoleta mkanganyiko wa
mawazo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top