Walimu wahofia ushirikina wilayani ukererwe.soma zaid
Ukerewe. Hofu ya vitendo vya ushirikina
imewafanya baadhi ya walimu wa Shule ya
Msingi Uhuru wilayani Ukerewe, Mkoa wa
Mwanza kushinikiza kuhamishwa.
Hali hiyo inatokana na mwalimu mwenzao,
Charles Bwatwa kuanguka ghafla na kupoteza
maisha akiwa njiani kurejea nyumbani.
Kabla ya kifo cha mwalimu Bwatwa kilichotokea
Oktoba 23, inadaiwa na walimu hao wamekuwa
wakifanyiwa ushirikina na hasa usiku wakiwa
wamelala.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Godwin Laurent
amesema tangu kifo cha mwenzao, walimu
wamekuwa wakiishi kwa hofu kiasi cha
kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kagera, Alfaxad
Kapole amelazimika kuitisha kikao cha pamoja
kati ya walimu na wakazi wa eneo hilo kujadili
madai ya kuwapo vitendo vya kishirikina.
Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Sengerema, Reginald Richard amesema kamati
maalumu imeundwa kuchunguza ukweli wa
jambo hilo ambalo limekuwa kikwazo cha utoaji
elimu kwa wanafunzi shuleni hapo.
0 comments :
Post a Comment