Breaking News
Loading...

Advert

Tuesday, November 1, 2016

Mwalimu akithaminiwa Elimu yetu itapanda chati.soma zaid

Mwaka 1966, Mwalimu Julius Nyerere alisema,
nanukuu.
“Wale wenye wajibu wa kufanya kazi na vijana
wa umri mdogo wana nguvu kubwa zisizozidiwa
na nguvu za yeyote yule kwa kutilia maanani hali
ya baadaye ya jamii yetu. Nguvu hizi zipo katika
makundi mawili, wazazi na walimu.”
Ukisoma hotuba zake nyingi, zimezungumzia kwa
kina masuala ya elimu kama mkombozi. Mwalimu
alieleza wazi kuwa, lengo la kwanza la elimu ni
kumkomboa mtu binafsi na taifa kutoka kwenye
kutegemea mataifa yaliyoendelea kiuchumi na
kiutamaduni.
Aidha, elimu inapaswa kumjengea mhitimu
maarifa, stadi na uwezo wa kukabiliana na
changamoto za maisha halisi anayoishi.
Katika kufanikisha lengo hili la elimu, mwalimu
alitaja katika nukuu hapo juu kuwa kuna makundi
mawili ambayo yana nguvu kubwa ya kuwafanya
wanafunzi kufikia malengo ya kuwapo shuleni.
Makundi haya ni wazazi na walimu.
Tafiti nyingi zilizofanyika katika kubaini sababu
za kushuka kwa ubora wa elimu zimekuwa
zikijikita katika kuangalia masuala kama
miundombinu isiyofaa ya kufundishia na
kujifunzia. Ni tafiti chache zilizolenga kuangalia
ubora wa walimu na mazingira yanayomzunguka.
Pia, tafiti hizo zinaonyesha wazi kuwa watoto
wetu hawajifunzi licha ya kuwa wanakwenda
shuleni. Kwa mfano, siyo jambo la kushanganza
kuona watoto wakimaliza darasa la saba bila
kujua kusoma na kuandika.
Jitihada zilizofanyika kujaribu kuinua kiwango cha
ubora wa elimu haziwezi kupuuzwa hata kidogo.
Serikali na wadau mbalimbali wamekuwa
wakifanya jitihada kubwa kuinua kiwango cha
ubora wa elimu yetu, lakini bado hatujaweza
kupata matokeo yanayotakiwa kama ambavyo
wadau wengi walitarajia.
Lazima tukubali kutafuta mzizi halisi wa tatizo la
kushuka kwa elimu yetu. Pengine tatizo
linafahamika lakini nia ya kushughulikia tatizo
siyo makini.
Kimsingi, tumechelewa kushugulikia kiini cha
tatizo kiasi kwamba Tanzania ya viwanda na ya
uchumi wa kati tunayoitaka kufikia mwaka 2025,
inaweza kuishia midomoni kama hatutaamua
kuchukua hatua mapema.
Wadau wengi wa elimu wameshasema kuwa
kuwathamini walimu ni moja ya hatua ya
kurejesha ari ya ufundishaji kama ilivyokuwa
miaka ya nyuma, yaani enzi za Mwalimu Nyerere.
Kuanzia ngazi ya taifa mpaka familia, walimu
hawaonekani tena kama watu muhimu;
wanachukuliwa kama watu maskini waliokosa
cha kufanya na ndiyo maana wapo huko.
Mwalimu mmoja aliwahi kusema: “Kuna wakati
wanafunzi wananiuliza, “Mwalimu, una akili, lakini
sasa kwa nini uliamua kuwa mwalimu?” Maswali
ya aina hii yanakera. Ina maana wanaamini
mwalimu ni mtu aliyefeli, asiye na akili.
‘’Ninapowaambia, nilipenda tu kuwa mwalimu”,
wananiambia huoni kwamba unachelewa katika
maisha? Haya ndiyo maisha tunayoishi katika
shule hii.’’
Ni dhahiri kuwa huu ndiyo mzizi wa tatizo la
kushuka kwa ubora elimu yetu. Miundombinu ni
muhimu katika kujifunza na kufundisha, lakini
pasipo walimu bora wenye moyo na hamasa ya
kufundisha kamwe hatutofikia elimu bora
tunayoitaka.
Utafiti uliofanywa na shirika la HakiElimu mwaka
2011 usemao: Je? Walimu wana sifa za ualimu
na hamasa ya kufundisha?, pamoja na mambo
mengine ulibianisha kuwa mwalimu kuwa na sifa
nzuri za kitaaluma pekee bila kuwa na hamasa
na moyo wa kujitolea hakusababishi kiwango cha
ufaulu wa mwanafunzi kitaaluma kuimarika’
Benedicta Mrema ni ofisa programu Idara ya
Habari na Utetezi, HakiElimu media@
hakielimu.org.chanzo mwananch

0 comments :

Post a Comment

Back To Top