Bunduki 11 zakamatwa nyumbani kwa Mubunge Dar.
Dar es Salaam. Kikosi kazi maalumu
kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo
sugu la ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo
zinasadikiwa kutumika kufanya ujangili na
kukamata watu wanne zaidi.
Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti
hili kuwa bunduki hizo zilikamatwa nyumbani kwa
mbunge wa CCM (jina tunalihifadhi) ambaye
bado anasakwa na kikosi kazi hicho.
Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya
Rais John Magufuli kutaja jina la mtu anayeitwa
Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu
wakati alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili
na Utalii na kushuhudia pembe 50 za ndovu
zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo.
Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita
“vijana” waendelee na kazi yao ya kukamata
wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali
ipo na kuwataka wasiogope mtu yeyote yule.chanzo mwananch
0 comments :
Post a Comment