Breaking News
Loading...

Advert

Monday, November 14, 2016

NSSF walipana bil.10/-posho za safari.soma zaid

NSSF walipana bil. 10/- posho za safari
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
lilitumia zaidi ya Sh. bilioni 10 kwa mwaka
kulipa posho za safari kwa wafanyakazi wake.
Kwa mujibu wa taarifa ya utedaji kazi wa NSSF
kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, ambayo
Nipashe inayo nakala yake, shirika hilo lilitumia
jumla ya Sh. bilioni 10.1 kulipa posho ya safari
kama moja ya vipengele vya gharama za
uendeshaji katika mwaka ulioishia Juni 2015.
Kiasi hicho kilikuwa ni ongezeko la Sh. bilioni
1.05 kulinganisha na mwaka uliotangulia.
Ripoti ya NSSF kwa mwaka wa fedha wa
2014/2015 iliwasilishwa kwa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mapema
mwaka huu na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,
Profesa Godius Kahyarara.
Chanzo: NIPASHE

0 comments :

Post a Comment

Back To Top