Polisi ashikiliwa kwa tuma ya kuficha meno ya tembo yenye uzito wa kilo 32.soma zaid
Ashikiliwa Polisi kwa meno ya tembo
kilo 32
POLISI mkoani Simiyu, Oliver Paschal (39),
mkazi wa Kijiji cha Ipililo katika Kata ya
Mwagala wilayani Maswa, amekamatwa kwa tuhuma za
kukutwa na meno ya tembo yenye uzito wa kilo
32 akiwa ameyaficha uvunguni mwa kitanda
chake.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa,
Onesmo Lyanga alisema baada ya kupata
taarifa za kiintelenjinsia, walimkamata
mwanamke huyo akiwa na pembe mbili za
ndovu alizokuwa amezificha chini ya uvungu
katika chumba alichokuwa akiishi.
Kamanda Lyanga alisema mwanamke huyo
alikamatwa Novemba 11, mwaka huu saa tisa
alasiri na kueleza kuwa alikamatwa na meno
hayo yenye uzito wa kilo 32 katika chumba
alichokuwa amepanga kwenye nyumba ya
Edward Malanda.
Aidha, kamanda huyo amesema kesi zaidi ya 86
zinazohusu ujangili zimesharipotiwa kuanzia
Januari hadi Septemba 2015, wakati kesi 69
zimesharipotiwa Polisi kuanzia Januari hadi
Septemba mwaka huu.
Katika hatua nyingine, jeshi hilo linawashikilia
watu wanane kwa kosa la kujichukulia sheria
mkononi kwa kumpiga na kumuua kwa mawe na
marungu, Manoni Elisha (38), mkazi wa Kijiji cha
Ngasamo wakimtuhumu kuwa ni mwizi.
Lyanga alisema saa 3 usiku katika baa ya
Manchester iliyopo Ngasamo wilayani Busega,
watuhumiwa hao walimuua mtu huyo kwa
tuhuma za makosa mbalimbali, ikiwemo wizi wa
kondoo kwa kesi namba NGAS/IR/49/2016
ambayo alikuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi.
0 comments :
Post a Comment