Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, December 7, 2016

Rais Obama aondoka Ikulu akishauri bangi iwe ruksa kama sigara.soma zaid


Rais Obama aondoka Ikulu akishauri bangi iwe
ruksa kama sigara, pombe
RAIS wa Marekani anayemaliza muda wake,
Barack Obama, amesema anadhani matumizi ya
bangi yaruhusiwe lakini udhibiti wake ufanyike
kama ilivyo katika matumizi ya sigara au pombe.
Hata hivyo, pamoja na mtazamo wake huo
kuhusu bangi, kiongozi huyo amesema hawezi
kulipigia debe suala hilo katika siku zake
zilizosalia katika Ikulu ya Marekani – White
House lakini yuko tayari kutumia muda wake
kama raia wengine wa taifa lake kuongoza
mijadala ya suala hilo.
Katika mahojiano yake na Jarida la Rolling Stone
wiki iliyopita – mahojiano yaliyoitwa ya kuaga
(exit interview), Obama amesema matumizi ya
bangi hayapaswi kufanywa kuwa kosa la jinai bali
yachukuliwa kama kosa la kiafya pale tu mhusika
anapozidisha matumizi yake hadi kupata
madhara ya kupindukia (addiction).
Kwa mujibu wa Obama, si busara kwa hali ilivyo
sasa nchini humo ambapo baadhi ya majimbo
yamekuwa na sheria inayoruhusu matumizi ya
bangi na mengine yakipinga matumizi hayo – hali
hiyo ikijitokeza katika taifa moja.
Kwa hiyo, anasema bangi iachwe kama ilivyo
kwa pombe na sigara lakini tu kuwekwe masharti
ya kitaifa kuhusu tahadhari za kiafya.
"Ni suala tete kwa Idara ya Sheria au Wakala wa
Usimamizi wa Sheria za Matumizi ya Dawa
kusimamia kikamilifu sheria hizi zilizoigawa nchi
vipande vipande kisheria– kwamba katika jimbo
moja suala hilo si kosa kisheria lakini ukipatikana
na hatia katika jimbo jingine ndani ya nchi hiyo
hiyo kwa suala hilo hilo unaweza kufungwa jela
miaka 20," alisema Obama.
Kwa sasa matumizi ya bangi kwa ajili ya
kujiburudisha yamehalalishwa kisheria katika
majimbo nane nchini Marekani na kwingine
hutumika kama dawa kwa ajili ya tiba.
Majimbo hayo ni pamoja na California,
Massachusetts na Nevada ambayo Novemba 8,
mwaka huu, wananchi wake walipiga kura
kuamua matumizi ya ‘mmea’ huo yawe halali
ama la. Katika majimbo mengine vimepitishwa
vifungu vya sheria vinavyotaka bangi iwe sehemu
ya dawa kwa ajili ya tiba.
Obama anatajwa kuvutiwa na kasi ya kuibuka
kwa mjadala kuhusu bangi kuruhusiwa kisheria
kama ilivyo wakati wa harakati za kutaka ruksa
ya kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kufunga
ndoa jambo lililotokea katika kipindi chake cha
urais.
"Kama ilivyowahi kuelezwa, nimewahi kuvuta
nikiwa mdogo, na niliona hiyo ni tabia mbaya
lakini vile vile haikuwa na tofauti kubwa na
sigara ambazo nazo zimekuwa nikivuta wakati
wa ujana na nilipoingia katika utu uzima. Sidhani
kama ina hatari kubwa kama ilivyo kwa pombe,"
aliwahi kusema Obama katika mahojiano
aliyopata kufanyiwa mwaka 2014.
"Kwa hiyo huu ni mjadala ambao umeiva sasa,"
aliliambia jarida la Rolling Stone, na kuongeza;
"..kama ilivyokuwa katika suala la ndoa za jinsia
moja. Tayari katika sehemu za nchi yetu hili
suala ni halali kisheria."
Inadaiwa kwamba kwa sasa watafiti wamebaini
kwamba matumizi ya bangi yanaungwa mkono na
idadi kubwa ya watu katika kipindi hiki kuliko
ilivyopata kuwa katika miaka ya nyuma nchini
Marekani.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa Septemba
mwaka huu, na taasisi ya Pew Research ya
Marekani, takriban asilimia 57 ya Wamarekani
wanaamini kuwa ni vizuri matumizi ya bangi
yahalalishwe kisheria ikilinganishwa na asilimia
37 wanaodhani kuwa iendelee kuwa haramu
kisheria.
Hali hiyo inatajwa kuwatofauti na ilivyokuwa
miaka 10 iliyopita, ambapo matokeo ya utafiti wa
aina hiyo yalionyesha mambo kuwa kinyume
kabisa – ikibainika asilimia 32 walikuwa
wakiunga mkono matumizi ya bangi kuwa halali
kisheria lakini asilimia 60 wakipinga.
Nafasi ya bangi kisheria
Nchini Marekani taasisi ya DEA inayohusika na
vita dhidi ya dawa za kulevya imeiweka bangi
katika kundi moja na dawa za kulevya aina ya
heroin na kwa mujibu wa taasisi hiyo, matumizi
ya bangi humweka mtu katika hatari kubwa ya
kufanya vitendo kinyume cha sheria.
Tangu miaka ya nyuma Obama amekuwa
mkosoaji mkubwa dhidi ya uamuzi wa taasisi hiyo
kuiweka bangi katika kundi moja na dawa za
kulevya aina ya heroin.
Mwaka 2014 katika mahojiano yake na gazeti la
New Yorker, alisema anadhani matumizi ya bangi
hayana madhara makubwa kama ilivyo kwa
matumizi ya pombe.
Na katika mahojiano mengine aliyowahi kufanya
hivi karibuni na mwanahabari Bill Maher, Obama
alisema; "Marekani inahitaji mjadala makini zaidi
kuhusu namna gani hasa suala la bangi na sheria
nyingine dhidi ya dawa za kulevya zinavyoweza
kupatiwa suluhu katika udhibiti."
Lakini kwa mujibu wa Rais Obama, kwa sasa hali
ya kisiasa haimpi nafasi ya kuwa mpiga debe wa
moja kwa moja wa harakati za kuhalalisha
matumizi ya bangi kisheria, ingawa pia, kwa
nafasi yake kama raia wengine, anasema
anaweza kusaidia katika mjadala wa suala hilo

0 comments :

Post a Comment

Back To Top