Chui aibuka na kupotea hospital ya mkoa wa Iringa.soma zaid
AMA kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya
firauni.... Katika hali isiyotarajiwa chui wa ajabu
amezua taharuki kubwa kwa wagonjwa na
wauguzi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa baada ya mnyama huyo kuibuka katika
mazingira ya kutatanisha.
Akizungumzia juu ya tukio hilo muunguzi
mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa
Iringa Rustica Tung’ombe alisema tukio hilo
limetokea majira ya saa 7 na saa 8 usiku wa
kuamkia leo Jumatano na kwamba chui huyu
alionekana nje eneo la wodi namba 6 .
Alisema kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na
muuguzi msimamizi wa zamu usiku ni kwamba
wanawake ambao walikuwa wakitoka
kunyonyesha watoto wao wodini walikimbia huku
wakipiga kelele za kuomba msaada baada ya
kukutana na chui huyo.
"Kulikuwa na kundi la kwanza la akina mama
waliotoka kunyonyesha watoto wao lilipita eneo
hilo na kundi la pili lilifuata na mwanamke mmoja
kati yao alikuwa nyuma akifuata wenzake na
ndipo alipomshuhudia chui huyo na kuanza
kupiga kelele ……wauguzi walipochungulia
madirishani walipata uhakika kuwa mnyama huyo
ni chui ", alisema.
Kutokana na kuwa na uhakika juu ya mnyama
huyo kuwa ni chui walilazimika kuomba msaada
kwa askari magereza ambao wamepakana na
hospitali hiyo kwa ajili ya kutoa msaada.
Alisema baada ya kufika askari magereza pamoja
na kundi kubwa la wananchi kwa ajili ya
kupambana na chui huyo ghafla mbwa aliibuka
nyuma ya chui huyo na kuanza kumfukuza chui
huyo ambaye aliruka ukuta wa uzio na kutoweka
kusikojulikana.
“Wakati askari magereza wanajiandaa
kupambana na chui huyo alitokea mbwa ambaye
kweli hatujui alitokea wapi na kuanza kumfuatilia
chui huyo ….. hili ni tukio la aina yake na
halijapata kutokea katika Hospitali hii maana
hapa ni mjini na hatujui chui huyu kafikaje hapa
0 comments :
Post a Comment