January 21, 2025
Breaking News
Loading...

Advert

Wednesday, January 25, 2017

Utawa wa Trump umeanza kuwa sumu kwa nchi za kiislamu hiki ndicho alichokifanya.soma zaid

Haijapita wiki moja toka Donald Trump aapishwe
kuwa Rais wa 45 wa Marekani na kukabidhiwa
ofisi, leo BBC wameripoti kwamba raia takriban
90 wa Somalia na wawili wa Kenya
wameondolewa kutoka Marekani.
Serikali ya Kenya imethibitisha kwamba raia wote
hao wamewasili katika uwanja wa kimataifa wa
Jomo Kenyatta Nairobi ambapo msemaji wa
serikali ya Kenya Eric Kiraithe amesema raia hao
wa Somalia watasafirishwa moja kwa moja hadi
Mogadishu.
“Ni watu 90 kulingana na habari ambazo
tulipewa, na wakati unaondolewa nchi fulani
kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi
kwenu,” kuhusu sababu iliyowafanya kuondolewa,
Kiraithe amesema: “Inategemea sheria za nchi
ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),”
Trump alisema Jumatano itakuwa siku muhimu
kwa usalama wa Marekani ambapo anatarajiwa
kuweka masharti makali kwa raia wa mataifa
saba ya Mashariki ya Kati na Afrika yenye idadi
kubwa ya Waislamu wanaotafuta vibali vya
kwenda Marekani.
Nchi hizo ni Syria, Iraq, Iran, Libya, Somalia,
Sudan na Yemen ambapo kama unakumbuka
wakati wa kampeni yake ya urais, Donald Trump
aliahidi kufanyia mageuzi suala la uhamiaji
Marekani.
Aligusia ujenzi wa ukuta kati ya Mexico na
Marekani kuzuia wahamiaji haramu na kuwapiga
marufuku Waislamu kuingia katika taifa hilo kama
sehemu ya vita dhidi ya ugaidi lakini baadae
alibadili msimamo kidogo na kufafanua kwamba
watakachofanyiwa Waislamu ni kufanyiwa
ukaguzi mkali kabla ya kuruhusiwa kuingia
Marekani.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top