Home
Unlabelled
jeshi la polisi zanzibar linaendelea kuwahoji watuhumiwa 42 wa dawa za kulevya.soma zaid
jeshi la polisi zanzibar linaendelea kuwahoji watuhumiwa 42 wa dawa za kulevya.soma zaid
hatimae kuvuuka maji hadi viasiwani Zanzibar.
Mkoa wa Mjini Magharib Unguja jeshi la polisi linaendelea na mahojiano na watuhumiwa 42 wa madawa ya kulevya na
kuwafanyia upekuzi wa nyumba zao.
Akizungumza na blog ya habrikwanza Kamishna msaidizi
mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa mjini magharib Unguja Hassan Nassir Ali.
Aliamesema wanaendelea kuwahoji watuhumiwa hao,ingawa hakua tayari kusema niniwamewakuta nacho na kuahidi taarifa rasmi itatolewa hapo badae.
Alieleza kuwa jeshi hilo limeanza harakati hizo kufuatia kauli za Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Mh,John Pombe Maagufuli ambae ndie amriri jeshi mkuu wa Nchi katika kupambana na dawa za kulevya.
‘’Tunawaita na kuwahoji watuhumiwa na kisha kufanya upekuzi kwenye nyumba zao ingawa ni mapema kusema nini tumegundua’’alisema Afisa huyo wa juu wa polisi.
Pamoja nahayo ameiasa jamii kutoa ushirikiano wa kina na jeshi hilo mara wanapogundua vitendo vya aina hio kwenye maeneo yao.
Alieleza kuwa kuna tatizo kubwa linalotokana na jamii hususani wananchi wa Zanzibar kila mmoja kujifanya anajua licha ya kuwa sheria ipo na inaelekeza kila kitu kwenye maisha yetu.
Aliasa jamii kuacha tabia ya kulihusisha jeshi hilo na rushwa na anapenda kuihakikishia jamii kuwa wanafanya kazi kwa weledi mkubwa .
‘’Kuna baadhi ya watu wamekuwa mstari wa mbele
kulalamika watuhumiwa tunapowapa dhamani licha ya kuwa ni haki yao kisheria,jamii inapaswa kujua dhamana ni haki ya kila mtu inategemea na tuhuma wenyewe’’alifafanua zaidi Nassir.
Akitolea ufafanuzi zaidi kamishna msaidi huyo aliesema mara watakapomaliza upelelezi wao na wale wote watakaogundulika na kuonekana na hatia watafikishwa mahakamani kusomewa kesi zao.
0 comments :
Post a Comment