Msanii Wema Sepetu anatalajia kujiunga rasimi CHADEMA hii leo.soma zaid
CHADEMA kupitia Mwenyekiti wa Chama
Taifa Freeman Mbowe, baada ya kesi ya
kikatiba namba 1 ya mwaka 2017
inayotarajiwa kuwasilishwa Mahakama
Kuu leo, kitazungumza kwa umma kupitia
waandishi wa habari na kuwakaribisha
wanachama wapya waliojiunga leo
akiwemo msanii Wema Sepetu.
Mbowe na Lissu leo wanawasilisha ile
hati ya mashitaka iliyorekebishwa na
kumuongeza Mwanasheria Mkuu. Wema
Sepetu yupo Katikati ya Esther Bulaya na
Mbowe hii leo. Kutoka Mahakama Kuu:
Kesi ya Mbowe dhidi ya RC Makonda, RPC
Sirro na ZCO Wambura
Baada ya hapa Mbowe ataongea na
Waandishi.
Ikumbukwe kwamba Lissu ambaye pia ni
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA)
na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, jana
alijitokeza mahakamani kuwa wakili wa
Wema na wenzake wawili akiwamo
mfanyakazi wa ndani. Msanii maarufu wa
fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu
anakabiliwa na kesi ya kukutwa na bangi.
Kesi hiyo ya Wema iliahirishwa hadi
Machi 15.
0 comments :
Post a Comment