Home
Unlabelled
Rais Trump amesain upya sheria ya kupinga wahamiqji wa nchi sita za kiislam kuingia Marekani.soma zaid
Rais Trump amesain upya sheria ya kupinga wahamiqji wa nchi sita za kiislam kuingia Marekani.soma zaid
Rais wa Marekani, Donald Trump ametia saini sheria mpya ya kuzuia wahamiaji kutoka nchi sita za kiislamu kuingia Marekani, katika sheria iliyotolewa mwanzoni na kuzuiwa na mahakama ilizitaja nchi saba, lakini kwasasa Iraq imeondolewa kwenye orodha hiyo.
Serikali ya Marekani imesema nchi zilizo orodheshwa zinafadhili ugaidi au zimeshindwa kupambana na magaidi wanaofanya shughuli zao ndani ya nchi zao.
Aidha, Nihad Awad wa Baraza la Kiislamu nchini Marekani linalotafuta kujenga mtazamo chanya wa dini ya kiislamu nchini humo, amesema watapambana dhidi ya Amri hiyo
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika linalotetea haki za wamarekani " American Civil Liberties Union "Lee Gelernt amesisitiza kuwa sheria hiyo itaiingiza Marekani kwenye matatizo.
''Hatufikirii kuwa sheria hii ni muhimu kwa usalama wa taifa, lakini si sisi tunaosema hivyo , ni wataalam wa masuala ya usalama na wanadiplomasia wanaoheshimika kutoka kwenye uongozi wa Democratic na Republican ambao mwanzoni walichukua hatua za kufungua kesi mahakamani kupinga sheria hii wakisema haita tufanya kuwa salama,"amesema Lee Gelernt.
Nchi zilizoorodheshwa kwenye sheria hiyo mpya ya Donald Trump ni Iran, Sudan, Syria, Libya, Somalia na Yemen. aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jeff Sessions ameviambia vyombo vya habari kuwa nchi tatu kati ya zilizotajwa zinafadhili ugaidi na nyingine tatu zimeshindwa kabisa kupambana na wanamgambo kama vile Islamic State na Al Qaeda
0 comments :
Post a Comment