Breaking News
Loading...

Advert

Monday, March 6, 2017

Ujio wa serikali waigusa Udom.

Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kimewapa watumishi wake wanaoishi eneo la Kisasa maarufu nyumba 300 miezi mitatu kujaza upya maombi ya nyumba, lengo likiwa ni kuwawezesha kukatwa asilimia 10 ya mshahara kama kanuni za utumishi zinavyoelekeza. Akizungumza ofisini kwake jana, Naibu Makamu Mkuu wa Udom (Mipango, Fedha na Utawala), Profesa Ahmed Mohamed Ame alisema habari zinazoenezwa katika mitandao ni za uongo na kwamba hakuna profesa anayefukuzwa katika nyumba. “Muda wote hawa wanaokaa katika nyumba hizi wamekuwa wakikaa bure tangu mwaka 2007. Kilipoanzishwa chuo hiki iliamuliwa wafanyakazi wakae bure kama motisha kulingana na mazingira ya wakati ule,” alisema Profesa Ame. Hivi karibuni kumekuwa na taarifa katika mitandao ya jamii kuwa watumishi wa chuo hicho, wameanza kufukuzwa kwenye nyumba walizokuwa wanaishi tangu mwaka 2007 ili kuwapisha watumishi wa Serikali wanaohamia mjini hapa, jambo ambalo limewaathiri kisaikolojia. Hata hivyo, alisema sasa kuna ongezeko la wafanyakazi kutoka 200 wakati chuo kilipoanzishwa hadi 1,407 na kwamba, imefika wakati wafanyakazi wote kutendewa haki kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top