Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, April 20, 2017

Apandishwa kizimbani baada ya kukutwa na kobe 100.soma zaid

MKURUGENZI wa Kampuni ya Afrilulu, Antony Gulfer (47) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya kukutwa nyara za serikali, ambazo ni kobe zaidi ya 100 wenye thamani ya Sh milioni 18.3. Gulfer ambaye ni raia wa Australia, alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali, Batilda Mushi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha. Mushi alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la kukutwa na nyara hizo za serikali kinyume na sheria ya wanyamapori. Alidai kuwa Machi 10, mwaka huu maeneo ya Kilomoni Kunduchi jijini Dar es Salaam, Gulfer alikutwa na nyara za serikali, ikiwemo kobe wanne aina ya tinged, pia kobe 108 aina ya Leopard na wengine wanne aina ya Aldabra. Inadaiwa kuwa kobe wote hao wana thamani ya dola za Marekani 8,190, sawa na Sh milioni 18.3. Mushi alieleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo, haujakamilika na anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Hakimu Mkeha alisema kuwa mahakama hiyo, haina mamlaka ya kuhusu dhamana na kwamba mshtakiwa anaweza kwenda kuomba Mahakama Kuu. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 2, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top