Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, April 20, 2017

Wabunge waendelea kuchezeana.soma zaid

Dodoma. Mazoea ya baadhi ya wabunge kuomba mwongozo wa kiti cha spika kuzima hoja za wabunge wenzao, jana uliibuka tena baada ya Mbunge wa Makambako, Deo Sanga kuomba mwongozo uliozima hoja ya kutaja majina ya wabunge 11 wanaodaiwa kutaka kutekwa. Sanga aliomba mwongozo wa Spika kwa kutumia Kanuni 68 (7) pamoja na 64 A,B,C, alisema ndani ya Bunge yameongelewa mambo yanayohusu mahakama, usalama, mauaji na kutekwa. “Nilikuwa nadhani kupitia kanuni hizi naomba mwongozo wako nini kazi ya Bunge mheshimiwa naibu spika?” alihoji. Mwongozo huo uliibuka baada ya Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Angelina Malembeka kuwataka wabunge waliosema kuna orodha ya wabunge 11 wanaotakiwa kutekwa kuwataja majina yao. Hoja ya Malembeka ilimlenga Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ambaye siku za karibuni aliliambia Bunge kwamba ameambiwa na mmoja wa mawaziri kuwa kuna wabunge 11 watatekwa na Usalama wa Taifa. Hata hivyo, mwongozo wa spika ulioombwa na Sanga ulizima kiu ya Malembeka aliyetaka kumbana Bashe ataje majina ya wabunge hao 11, badala ya kutaja idadi pekee. Akijibu mwongozo wa Sanga, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson aliamua kupiga marufuku masuala ya Usalama wa Taifa kujadiliwa bungeni.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top