Ntoto wa darasa la kwanz mkoani Pwani ahofia kufa maji.
Mtoto wa darasa la kwanza mkoani
Pwani.anahofiwa kufa maji baada ya kuzama
mtoni wakati wakiogelea.
Mtoto wa darasa la kwanza katika shule ya
msingi Ubena Tarafa ya Chalinze mkoa wa Pwani
aliyefahamika kwa majina ya Karim Salum
anasadikika kufariki dunia baada ya kuzama
kwenye maji ya mto Ngerengere wakati akiogelea
na wenzake huku jitihada za kutafuta mwili wake
zikigonga mwamba kutokana na wananchi
kuutafuta mwili huo kwa zaidi ya siku mbili
mfululizo bila mafanikio.
ITV imeshuhudia wananchi wakiendelea na
jitihada za utafutaji wa mwili wa mtoto Karim
Salum anayesadikiwa kufa maji huku vijana
walioshuhudia mtoto huyo akizama ndani ya maji
wakieleza tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi
Alasiri wakati wakijaribu kuogelea ndani ya mto
huo.
Naye Babu wa mtoto huyo Bwana Issa
Bung’ombe ameeleza kusikitishwa na tukio hilo
na kwamba mtoto huyo aliaga nyumbani
akielekea mtoni kuchota maji ndipo kadhia hiyo
ilipomkuta.
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa kijiji cha
Bwawani Abdalah Seifu ameiomba serikali kupitia
vyombo vya uokoaji kuwasaidia kuongeza nguvu
ya kumtafuta mtoto huyo anaye sadikiwa kufa
maji ili kuokoa mwili wake.
0 comments :
Post a Comment