Breaking News
Loading...

Advert

Sunday, May 28, 2017

Ikulu yaijibu Acacia.soma zaid


Dar es Salaam. Uamuzi wa Serikali kuhusu suala
la usafirishaji wa mchanga wa madini,
utategemea ripoti ya kamati ya pili iliyoundwa na
Rais John Magufuli kuchunguza suala hilo.
Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa
Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Gerson Msigwa
ikiwa ni siku moja baada ya kampuni ya Acacia
kuitaka Serikali kuunda kamati huru kuchunguza
kiasi cha madini kwenye makontena yake 277
yaliyozuiwa bandarini.
Wiki iliyopita, Rais Magufuli alikabidhiwa ripoti na
kamati ya kwanza iliyoongozwa na Profesa
Abdulkarim Mruma ambayo ilibaini kuwa
makontena hayo yana tani 7.8 za dhahabu.
Pia, Acacia wanadai hawakupewa ripoti ya
kamati hiyo licha ya kutoa ushirikiano wakati wa
uchunguzi.
“Sijui chochote kuhusu hao Acacia kuomba
iundwe kamati huru, lakini tunasubiri ripoti ya
kamati ya pili iliyoundwa kuchunguza sakata hili
wampelekee ripoti Rais,” alisema Msigwa.
Wakati Ikulu ikisema hayo, Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe alizungumzia ripoti ya
kamati ya Profesa Mruma na kusema chanzo cha
hayo ni sheria mbovu za madini pamoja na
mikataba iliyotungwa katika kipindi cha utawala
wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais
Benjamin Mkapa. “Tanzania inaruhusu kupitishwa
kwa sheria mbovu na wizi halafu baadaye
wanapiga kelele, wapinzani tunasema sheria zote
lazima zifumuliwe na kupangwa upya,” alisema.
Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai alionyesha
shaka kuwa ni lazima Taifa litaingia kwenye
migogoro mikubwa ya kidiplomasia kutokana na
ukiukwaji wa sheria unaofanywa ikiwamo sakata
la mchanga huo.
Alisema itachukua muda mrefu kwa wawekezaji
kuiamini tena Tanzania na kuja kuwekeza kwa
kuwa hata waliopo wameanza kuondoka.
Pia, Mbowe alisema kuna tetesi kuwa uchunguzi
huo ambao ulimng’oa Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo una upungufu
mwingi.
Suala la fedha nalo limeibuka katika sakata hilo.
Akizungumzia suala hilo, aliyekuwa mjumbe wa
Mpango wa Uhamasishaji wa Uwazi katika
Mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (Teiti),
Bubelwa Kaiza alisema ipo haja ya kupitiwa upya
kwa taarifa za fedha za kampuni za madini
ambazo zilikuwa zikiwasilishwa.
Kaiza alisema kwa mujibu wa ripoti ya kamati ya
kuchunguza mchanga wa madini iliyowasilishwa
siku chache zilizopita ni wazi kampuni hizo
hazikuwa zikitoa taarifa sahihi.
Alisema Teiti ilikuwa inapitia taarifa za fedha
ambazo zilikuwa zinawasilishwa kwa hiari na
kampuni husika na si kuchunguzwa, hivyo upo
uwezekano walikuwa wanatumia mwanya huo
kutoa taarifa za uongo.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top