Mkuu wa mkoa wa shinyanga leo ameruhusiwa kuingia ndani ya mdogi.soma zaid
Kahama. Baada ya kuzuiwa kuingia mgodini jana
na kuamua kuweka ulinzi wa polisi kuhakikisha
hakuna anayeingia wala kutoka, Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga, Zainab Tellack leo ametembelea
mgodi huo na kupiga marufuku mgodi huo
kuyeyusha wala kusafirisha dhahabu hadi kibali
cha serikali.
Akizungumza na Mwananchi mara baada ya
kufanikiwa kuingia mgodini humo leo alfajiri,
Mkuu huyo wa mkoa amesema shughuli hizo
zitarejea baada ya serikali kupeleka Maofisa
wapya wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini, TMAA
kusimamia uzalishaji, ukaguzi na usafirishaji.
Katika hatua nyingine, uongozi wa mgodi wa
Bulyanhulu kupitia kwa Meneja wake wa Ufanisi
na Maendeleo ya Jamii, Elias Kasitila umetoa
sababu za kiongozi huyo kushindwa kuingia
kwenye eneo maalum la kuhifadhi dhahabu kuwa
ni masuala ya kiulinzi kutokana milango yake
kufunguka kwa muda wa saa 24, ulitegeshwa
kufunguka saa 12:00 alfajiri leo.
0 comments :
Post a Comment