Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 4, 2017

Kauli ya Rais Magufuri yaleta neema Tanesco.soma zaid

Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) Mkoa wa Ilala limekusanya Sh2 bilioni
kutoka katika taasisi za Serikali zilizokuwa
zinadaiwa na shirika hilo.
Deni hilo limekusanywa tangu Rais John Magufuli
atoe agizo la kulitaka shirika hilo kuwakatia
umeme wadaiwa sugu.
Akizungumza leo Meneja wa Tanesco Mkoa wa
Ilala, Athanasius Nangali amesema wadaiwa sugu
walikuwa wanadaiwa jumla ya Sh 7 bilioni.
Taasisi za Serikali zilikuwa zinadaiwa Sh 6 bilioni
na sasa wamelipa Sh 2 bilioni na zimebaki Sh 4
bilioni.
"Tumeingia mkataba na taasisi za serikali wa
namna ya kulipa madeni yao na makubaliano ni
kuwa watamaliza deni lililobaki mwezi huu hadi
mwezi ujao," amesema.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top