Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 4, 2017

Kigogo asimamishwa kazi kwa kupora hekari 4,000.za aridhi. Soma zaid

Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
amemsimamisha kazi Afisa Mipango
Miji wa Lindi, Castory Manase Nkuli
baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji
vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na
kumilikisha kampuni ya Azimio
Housing Estate kinyume cha sheria.
View attachment 504370
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu
Castory Manase Nkuli Afisa Mipango
Miji kwa tuhuma za kumilikisha ardhi
kinyume cha sheria
Waziri Lukuvi aligundua hayo baada ya
kuona utaratibu wa umilikishaji wa
ardhi haukufuatwa na badala yake
kuonekana kuwa na mianya ya rushwa
kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa
kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa
kwa kampuni ya Azimio ambapo
kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo
itoke kwa idhini ya Rais.
Afisa Mipango Miji huyo aligundulika
kuwa na kosa la kughushi kwa
kujifanya ni Afisa ardhi baada ya
kuandika barua na kuisaini kwa niaba
ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa
Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni
ya Azimio Housing Estate ambalo pia
ni kosa kisheria.
“Kama nyie hamna uwezo wa
kumfukuza kazi basi mie
namsimamisha kazi kuanzia leo hafai
kuwa mtumishi wa serkali” alisema
Lukuvi huku akiagiza eneo hilo lirudi
na kuwa mali ya serikali. Sasa hiyo
ardhi lazima irudi itakua mali ya
serikali kuanzia leo”.
Akithibitisha makosa hayo Kaimu
Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji
kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate
Senje amesema kwamba utaratibu wa
umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa
ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo
hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada
ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na
wana kijiji.
Chanzo: Bongo 5
Mh. Waziri Lukuvi hilo likampuni la
Azimio Housing Estate nalo ni
lakunchunguzwa kwa kina sana,
Limekaa kidili

0 comments :

Post a Comment

Back To Top