Mapenzi mubashara: Binti wa mfalme wa Japani aacha cheo aolewe na mpenzi wake wa kawaida.soma zaid
Mjukuu wa kike wa Mfalme Akihito wa Japan,
Binti Mfalme Mako, amekubali kupoteza hadhi na
haki zote za umalkia ili aweze kuolewa na
mpenzi wake, waliyekutana tangu akiwa chuo
kikuu.
Taarifa zilizotangazwa jana na kituo cha
televisheni cha umma, NHK, juu ya uamuzi huo
wa Binti Mfalme Mako zimeitikisa Japan nzima.
Magazeti, televisheni, redio na mitandao ya
kijamii imeamkia Jumatano ya leo ikiwa na
habari hiyo, huku uchumba rasmi ukitazamiwa
kutangazwa wiki chache kutoka sasa.
Mchumba wake, Kei Komuro, ni kijana wa miaka
25 aliyewahi kupewa jina la “Mwanamfalme wa
Bahari” na mashindano ya kushajiisha utalii hivi
karibuni.
Mwanamme huyo kutoka familia ya watu wa
kawaida, amezungumza na waandishi wa habari
muda mfupi uliopita, ambapo amekwepa kabisa
kuzungumzia suala la uchumba, akisema kuwa
atasema “pale tu muda utakapofika.”
Habari za uchumba huu zimezuwa mashaka
makubwa sio tu juu ya nafasi ya mwanamke
kwenye ukoo wa kifalme, bali pia mustakabali wa
ufalme huo, ambao kwa mara ya kwanza ndani
ya karne mbili zilizopita utachukuwa hatua ya
kumuondoa madarakani mfalme aliye hai katika
wakati ambapo warithi wa kiume ni wachache
sana.
Mako, ambaye pia ana umri wa miaka 25, ni binti
mkubwa wa Mwana Mfalme Akishino, ambaye ni
mtoto wa pili wa kiume wa Mfalme Akihito, na
kama ilivyo kwa wanafamilia wote wa kike wa
ufalme huo, anapoteza hadhi na haki yake ya
kifalme kwa kuolewa na mtu wa kawaida,
kutokana na sheria zao.
Hata hivyo, sheria hiyo haiwahusu wanaume,
ambapo Akihito na wanawe wameowa watu wa
kawaida, na ambao sasa ni sehemu ya ufalme.chanzo zanzibar Daima
Share this:
0 comments :
Post a Comment