Breaking Newz #Meya wa jiji la Arusha akamatwa na polisi.soma zaid
Mstahiki Mayor wa Jiji , Paroko ,
Mchungaji , Waandishi wa habari 7 ,
wamekamatwa leo na Jeshi la Polisi
wakiwa Shuleni Lucky Vicent ambako
Mayor alialikwa na Umoja wa Shule
binafsi Tanzania , waliopenda kutoa rambi
rambi moja kwa moja kwa wafiwa badala
ya kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa .
Wazazi waliokuwa hapo wamepatwa na
taharuki kubwa baada ya kuona viongozi
hao wanachukuliwa bila sababu yoyote ya
msingi , mpaka sasa wako Polisi
wanaambiwa walikuwa na mikusanyiko
isiyo halali .
Nafikiri tunachoka sana . Mungu mpaka
lini mambo haya ?
=====
Wamiliki wa Shule Binafsi walioenda kutoa
rambirambi katika Shule ya Msingi ya
Lucky Vincent wakiwa na waandishi wa
habari wamewekwa chini ya ulinzi na
polisi shuleni.
Mwandishi wetu ambaye yuko eneo la
tukio hivi sasa ameeleza kuwa Mkuu wa
Upelelezi wa Wilaya Arusha ambaye
hajamtaja jina amewaambia kuwa wako
chini ya ulinzi kwa kosa la kufanya
mkusanyiko kinyume cha sheria.
Mwandishi wetu ameeleza kuwa katika
msafara huo pia yupo Meya wa Jiji la
Arusha, Kalist Lazaro, viongozi wa dini,
wazazi waliofiwa.chanzo mwananch
0 comments :
Post a Comment