Breaking News
Loading...

Advert

Monday, May 22, 2017

Ukatili w mauaji mkoan Singida Mtoto ameuwawa na kunyofolew badhi ya viungo vyake.soma zaid

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtoto
wa miaka 12, Dorcas Meshak mkazi wa
kitongoji cha Mbughantigha kijiji cha
Matongo tarafa ya Ikungi, ameuawa na
watu wasiojulikana na kunyofolewa
baadhi ya viungo vyake.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kaimu
Kamanda Jeshi la Polisi mkoani hapa,
SSP Isay Mbugh alisema Mei, 18 mwaka
huu saa sita mchana wakati ambao
Dorcas alipoondoka nyumbani kwao kwa
lengo la kwenda shambani kuchuma
mahindi, umbali wa kilometa 70.
Alisema mtoto huyo amenyofolewa macho
yote mawili, kukatwa matiti yote na
kuondolewa sehemu zake za siri.
“Mtoto Dorcas hakuweza kurudi nyumbani
kitendo kilichosababisha ipigwe yowe ili
watu wakusanyike kwa ajili ya kumtafuta.
Haikuchukua muda mrefu, mwili wa
Dorcas ulikutwa ukiwa umenyongwa hadi
kufa kwa kamba ya ngozi,” alisema.
Alisema uchunguzi wa awali umebaini
kuwa mauaji hayo yanahusishwa na imani
za ushirikina na hadi sasa hakuna watu
waliokamatwa kuhusiana na mauaji hayo.
Katika tukio la pili, Kaimu Kamanda
Mbugh, alisema watu wawili wamepoteza
maisha kufuatia kutokea ajali ya gari
anina ya Noah, tukio ambalo lilitokea Mei,
20 mwaka huu saa 6.45 mchana huko
katika kijiji cha Mwaja tarafa ya
Unyankumi Manispaa ya Singida.
“Ajali hiyo imehusisha noah T.402 DFH
iliyokuwa ikiendeshwa na Said Shaban
(33), na chanzo cha ajali ni mwendo kasi
kitendo kilichosababisha ashindwe
kulimudu. Waliofariki kwenye ajali hiyo,ni
Elia Daniel (34) mkulima kijiji cha
Mwankoko na mwanamke mmoja ambaye
jina wala makazi yake,hayajafahamika,”
alisema.
Aidha, aliwataja majeruhi wa ajali hiyo
kuwa ni Mratibu Elimu kata ya Mtamaa,
Nicodem Elias (45), Juma Ramadhan,
mwalimu Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi, Elia Bilau mkulima na mkazi
wa Magungumka Kapela Donad (28).
Kaimu kamanda huyo, alisema dereva wa
Noah hiyo Said Shaban anashikiliwa na
Jeshi la Polisi na upepelezi ukikamilika
atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili.
Chanzo: Mo Blog

0 comments :

Post a Comment

Back To Top