Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, May 18, 2017

Usafiri wa Treni umesimamishwa kutoka Dar kwenda Bara kuanzia leo tareh 18.soma zaid

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –
PRESS RELEASE
KUSIMAMISHWA HUDUMA YA TRENI ZA
ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO MEI
18, 2017
Uongozi Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
umetangaza kusimamishwa huduma ya
treni za abiria kutoka Dar es Salaam
kwenda bara kuanzia leo Mei 18, 2017
hadi itakapotangazwa tena.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya
kutokea uharibifu wa miundombinu ya reli
leo asubuhi kati ya stesheni za Ruvu na
Ruvu junction uliosababishwa na mvua
kubwa zinazonyeshwa maeneo hayo ya
mkoa wa Pwani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya kusitisha
huduma kwa muda treni ya abiria ya
deluxe iliokuwa iondoke Dar es Salaam
leo saa 2 asubuhi imefutwa na abiria
wametakliwa wafike stesheni ili
warejeshewe fedha zao za nauli.
Wakati huo huo Uongozi wa TRL tayari
umeelekea eneo la tukio ili kufanya
tathmini na kupanga mikakati ya haraka
kukarabati miundo mbinu husika likiwemo
daraja la Ruvu.
Aidha Uongozi umefafanua katika taarifa
yake kuwa katika kipindi cha mpito, treni
ya abiria kutoka Kigoma na Mwanza kuja
Dar es Salaam itaishia Morogoro hadi njia
ya reli kati ya Dar es Salaam na Morogoro
itakapofunguliwa tena.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
KampunI ya Reli Tanzania(TRL),
Mei 18, 2017
DAR ES SALAAM
Daraja la Ruvu reli ya kati limekatika.
Hakuna treni yoyote kutoka Dar au kuja
Dar itakayopita. Mungu tunusuru.chanzo jamii forums

0 comments :

Post a Comment

Back To Top