NJOMBE:Mwalimu afumaniwa akinya mapenzi na mwanafunzi Darasani.soma zaid
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe,
Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza
kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule
ya sekondari Wanike, iliyopo katika wilaya
hiyo baada ya kukamatwa akifanya
mapenzi na mwanafunzi wake darasani
usiku.
Kasinge ametoa agizo hilo baada ya
kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu
wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo
kuvuruga ushahidi kwa kupanga na
wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea
tofauti na tukio.
"Kuanzia wanafunzi waliotimuliwa
wahojiwe na polisi na wale wanafunzi
wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi
na mwalimu mwenyewe pia aendelee
kushikiliwa .Huyo ambaye anatuhumiwa
aendelee kushikiliwa na polisi mpaka
tupate majibu, kwa sababu akibaki nje
ataendelea kutengeneza mazingira ya
kutengeneza mtandao wa kutaka
kumsaidia na kupotosha ushaidi" alisema
Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge
Mbali na hilo shule ya sekondari ya
Wanging'ombe pamoja na Wanike
zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea
wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa
shule hizo wameweka wazi kuwa shule
hizo zinachangamoto ya walimu wa
sayansi ambao ni wachache ukilinganisha
na walimu wa masomo ya sanaa.
Chanzo: Mpekuzi
0 comments :
Post a Comment