Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, June 17, 2017

TETESI USAJIL WA SOKA ULAYA JUMAMOS.2017


*Kitendawili cha Ronaldo kigumu
*Arsenal kuvunja rekodi ya dunia ya usajili
*De Gea anatafuta nyumba Spain
Real Madrid imesema mshambuliaji wake
Cristiano Ronaldo hajaiambia klabu hiyo kuwa
anataka kuondoka (ABC).
Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa
Ureno hajapanga kurejea Spain baada ya
kucheza katika Kombe la Shirikisho linalofanyika
Urusi (Record).
Ronaldo alimwambia wakala wake Jorge Mendes
miezi miwili iliyopita kuwa anataka kuondoka
Madrid (AS).
Chelsea hawapo tayari kumpa mamlaka makubwa
Antonio Conte kwenye suala la usajili, huku
kukiwa na tetesi kuwa meneja huyo anazidi
kughadhabishwa na kutokuwepo na usajili
wowote (Guardian).
Lakini Chelsea wamesisitiza kuwa hawana
mpango wowote wa kumuachilia Conte aondoke
na watampa kila msaada katika suala la usajili,
huku mikataba ya wachezaji wanne ikiandaliwa
ukiwemo wa Romelu Lukaku, 23, na kitita cha
usajili huenda kikafikia pauni milioni 250 (Daily
Mirror).
Manchester City wamemkabidhi Pep Guardiola
pauni milioni 300 kwa ajili ya usajili, lakini City
hawataki kulipa pauni milioni 70 kumnunua beki
wa kati wa Southampton Virgil van Dijk, 25
(Manchester Evening News).
Arsenal wameripotiwa kupanda dau la kuvunja
rekodi ya dunia la zaidi ya pauni milioni 100
pamoja na Olivier Giroud ili kumsajili Kylian
Mbappe kutoka Monaco (Sun).
Chelsea hawana mpango wa kumruhusu Conte
aondoke, na watamkabidhi pauni milioni 250 za
usajili kuthibitisha hilo (Mirror).
Manchester United watamsajili winga Ivan Perisic
kwa pauni milioni 44 wiki chache zijazo (Mail).
David de Gea ameongeza juhudi za kutafuta
nyumba Spain wakati akijiandaa kuondoka
Manchester United (Star).
Michy Batshuayi atakataa kwenda West Ham,
huku akijaribu kujadili na Chelsea mustakbali
wake (Express).
Kipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma
amependekezwa kwenda Manchester United na
wakala wake Mino Raiola (Diario Gol).
Manchester United na Liverpool watalazimika
kutoa pauni milioni 50 iwapo wanataka kumsajili
kipa wa Leicester City Kasper Schmeichel (The
Sun).
Beki wa kati wa Roma Kostas Manolas anasakwa
na Chelsea kwa pauni milioni 42 (Sport FM 94.6
ya Ugiriki).
Manchester United na Juventus zitamfuatilia
kiungo wa Barcelona Andre Gomes (AS).
Klabu yoyote inayotaka kumsajili Cristiano
Ronaldo kutoka Real Madrid italazimika kutoa
euro milioni 400 (Gazzetta dello Sport).
Kiungo wa Monaco Tiemoue Bakayoko
amechagua kujiunga na Chelsea na kuzitosa
Manchester City na Manchester United (L’Eqipe).
Bayern Munich bado wanamfuatilia kiungo wa
Paris Saint Germain Marco Verratti, licha ya
kumsajili Corentin Tolisso kutoka Lyon (Bild).
Kipa wa akiba wa Manchester City Willy
Caballero, 35, anatarajiwa kuthibitishwa kuwa
usajili wa kwanza wa Chelsea wa msimu
(Evening Standard).
Tottenham wamewaambia Manchester United
kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 50
kumsajili kiungo Eric Dier, 23 (Daily Telegraph).
Arsenal watarejea tena Lyon wakiwa
wameongeza dau kufikia karibu pauni milioni 50
kutaka kumsajili Alexandre Lacazette, 26. Dau la
awali la pauni milioni 30 lilikataliwa msimu
uliopita (Daily Telegraph).
Lyon wapo katika mazungumzo ya kina ya
kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea
Bertrand Traore, ambaye alikuwa Ajax kwa
mkopo msimu uliopita (Evening Standard).
Beki wa kulia wa Juventus Dani Alves
ameshutumiwa vikali na mashabiki kwa kusema
Pablo Dybala, 23, anatakiwa kuondoka Juve
iwapo anataka kupata maendeleo katika soka (Il
Giornale).
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na
Manchester United Robin van Persie, 33,
anakaribia kuondoka Fenerbahce na kwenda
Feyneerd ya Uholanzi (FR12.nl).
West Ham wanataka kumsajili winga wa
Middlesbrough Adama Traore, 21, lakini
Middlesbrough wamesema hawana tatizo la
fedha (Teeside Gazette).
Inter Milan watataka pauni milioni 45 kutoka kwa
Manchester United wanaotaka kumsajili winga
Ivan Perisic, lakini United wanataka kutoa Pauni
milioni 30 (Manchester Evening News).
Kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Douglas
Costa, 26, anakaribia kuhamia Juventus kwa
kitita cha pauni milioni 26, ambapo amekubali
mkataba wa miaka mine (L’Equipe).
Arsenal wanatarajiwa kuwazidi kete Everton
katika kumsajili mshambuliaji wa AC Milan
M’Baye Niang, 22, ambaye alikuwa Watford kwa
mkopo msimu uliopita (Hertfordshire Mercury).
Birmingham bado wanasubiri jibu kutoka kwa
nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, 36,
ambaye amekubali dau lao la pauni 100,000 kwa
wiki (Daily Mirror).
Swansea bado wanazungumza na Galatasaray
kuhusu kuwauzia Bafetimbi Gomis, 31, ambaye
alikuwa Marseille kwa mkopo msimu uliopita
(Wales Online).
Hull na Ndwcastle zote zinamuania mshambuliaji
wa Chelsea Tammy Abraham, 19 kwa mkopo
(Sun).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara tu
zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa. Weekend njema nyote.
Tafadhali share tetesi hizi na wapenda soka
wote.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top