Breaking News
Loading...

Advert

Saturday, June 17, 2017

Uko tayari kulipwa sh.10milion kwa kuambukizwa kikohozi?


Southmpton. Je ni fedha kiasi gani zinaweza
kukushawishi kukubali kuambukizwa kikohozi ili
kusaidia uvumbuzi wa kisayansi?
Watafiti wa Chuo Kikuu cha Southampton
wamesema watampa pauni 3,526 (sawa na
Sh10.3 milioni) mtu yeyote atakayejitokeza ili
kukubali changamoto hiyo.
Lengo lao kubwa ni ili kutengeza chanjo bora ili
kuwalinda watoto na watu wazima ambao wapo
hatarini kuambukizwa ugonjwa huo.
Ili kusaidia ni sharti mtu awe na umri wa kati ya
miaka 18-45, awe na afya bora, awe tayari
kutengwa kwa siku 17 na kuimba.
Kikohozi ni ugonjwa unaoweza kuambukizwa kwa
haraka na huenezwa kupitia hewa ya kikohozi
kutoka kwa mtu ambaye ameambukizwa.
Kundi hilo la watafiti wa Chuo Kikuu cha
Southampton linataka kuwaambukiza watu walio
na afya nzuri kwa kuwawekea puani viini
vinavyosababisha maambukizi hayo na
kuwachunguza.
Baadhi ya watu waliojitolea watakuwa wagonjwa,
lakini wanasayansi wanawataka wale ambao
hawatakuwa na dalili zozote licha ya kuwekewa
viini hivyo katika pua zao.
Hatu hii inalenga kujua wale wenye kinga ya asili
ya ugonjwa huo.
Vilevile, wapo wanaobeba ugonjwa huo kwa siri
na huwaambukiza watu wengine, lakini huwa
hawaambukizwi.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top