Klabu ya Dar Yanga Afrika imempata msemaji mpya wa klabu( Dismas Ten).soma zaid
semaji mpya wa Yanga Dismas Ten.
Klabu ya Yanga leo imemtangaza rasmi
aliyekuwa afisa habari wa klabu ya soka ya
Mbeya City Bwana Dismas Ten kama afisa habari
wao baada ya kuingia nae mkataba leo.
Dismas anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
aliyekuwa afisa habari wa klabu hiyo Jerry Murro
ambaye mwaka jana 09 Julai 2016 alifungiwa na
Shirikisho la soka nchini kujihusisha na soka.
Nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Godlisten
Anderson Chicharito kama kaimu afisa habari
ambaye sasa ataendelea na nafasi hiyo chini ya
Dismas Ten.
“Tumeamua kuleta mapinduzi kwenye utoaji
habari kwenye klabu yetu na naamini kwa
muunganiko huu wa Dismas na Chicharito klabu
yetu itafanikiwa sana kupitia kitengo iki cha
Habari na mawasiliano kama vilabu vingine
vikubwa duniani.”-Boniface Mkwasa Katibu Mkuu
Yanga SC.
0 comments :
Post a Comment