Home
Unlabelled
Machangudoa waundiwa vikundi vya ulinzi.soma zaid
Machangudoa waundiwa vikundi vya ulinzi.soma zaid
Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wamelazimika kuunda vikundi vya ulinzi katika mitaa yao nyakati za usiku kwa lengo la kutokomeza biashara ya uchanguduo na uhalifu uliokithiri katika kata hiyo.
Hayo yamebainishwa na wananchi hao katika mkutano uliotishwa na diwani wa kata hiyo, Hawa Mushi, kwa lengo la kujadili changamoto zinazowakabili katika maeneo yao na kutoa maazimio.
Janeth Mbwambo, mkazi wa eneo hilo, amesema tatizo la machangudoa kuzagaa katika maeneo ya kata hiyo limekuwa kero nyakati za usiku pamoja na vijana wanaofanya uhalifu pia wamesababisha watu kuwa na hofu ya usalama wao.
Mkazi wa kata hiyo, Mary William, amesema pamoja na juhudi zinazofanywa za kuimarisha ulinzi bado hali imekuwa mbaya kwa kata yao huku akidai kuwa kama hawataimarisha ulinzi wao wenyewe tatizo hilo litaendelea kuwepo.
Diwani wa kata hiyo amesema wamejitahidi kupambana na uhalifu na machangudoa lakini bado tatizo limekuwa likiendelea na kwamba wataingia katika ulinzi wenyewe ili kukomesha kabisa jambo hilo.
“Tunaingia katika mapambano wenyewe ili kuwakabili machangudoa pamoja na uhalifu unaofanywa na watu kutoka nje ya kata yetu na si wakazi wa eneo husika, hali hiyo imeichafua sana kata yetu,” amesema Diwani Mushi.
Akijibu kero za wananchi hao kuhusu kelele za mziki nyakati za usiku, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema suala hilo limeshatolewa maelekezo kwa mkurugenzi wa manispaa hiyo.
Amesema kama mtu hataweza kufuata masharti ya kupiga muziki usiku, vyombo vyake vya muziki vitachukuliwa na kupelekwa katika halmashauri hiyo na akiendelea kukaidi atafungiwa na faini yake ni kiasi cha Sh.1 Millioni.
Akizungumzia suala la wafanyabiashara maarufu kama wamachinga Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Jaffar Michael, amesema suala lao limeshapitishwa bungeni kwamba ili waweze kutambulika wanatakiwa kila mmoja ajisajili.
Amesema jambo hilo litasaidia kuepusha migongano na itawaepushia kufukuzwa na kupigwa na baadhi ya mgambo, na sheria hiyo inatakiwa ianze Julai Mosi mwaka huu kwani watakuwa wanatambulika kisheria.
0 comments :
Post a Comment