Mahakama imemuachia huru Yusuph Manji .soma zaid
Mahakama ya Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi Mh.Cyprian Mkeha. Leo hukumu ya kesi ya matumizi ya Dawa za kulevya dhidi ya Mfanyabiashara Yusuf Manji itasomwa. Nitawajuza baada ya hakimu kumaliza... UPDATES: Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 6 mwezi wa 10, 2017 imemuachia huru mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa. Sababu kuu ni kuwa mtuhumiwa alikuwa na bado anatumia dawa mbalimbali kwa matibabu yake kulingana na maagizo ya daktari na dawa hizo zina elements za morphine ambayo pia inaweza kukutwa kwenye heroin kwahiyo maabara ya Mkemia Mkuu ingeenda mbele zaidi kujua morphine iliyokutwa kwa mtuhumiwa imetokana na nini. Hilo ndio limesababisha Manji kuachiwa HURU.
0 comments :
Post a Comment