Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Thursday, October 29, 2015
WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WAKISHANGILIA USHINDI KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA DAR ES SALAAM

WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WAKISHANGILIA USHINDI KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA DAR ES SALAAM


DR. JOHN POMBE MAGUFULI NDIYE RAIS MTEULE WA AWAMU YA 5 TANZANIA

DR. JOHN POMBE MAGUFULI NDIYE RAIS MTEULE WA AWAMU YA 5 TANZANIA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi -NEC imemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi - CCM, Dokta JOHN POMBE MAGUFULI kuwa mshindi wa Urais kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  NEC Jaji mstaafu DAMIAN LUBUVA amemtangaza Dokta MAGUFULI kuwa amepata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 akifuatiwa na Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA aliyepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97.

Mgombea ANNA ELISHA MGHWIRA wa Chama Cha ACT WAZALENDO amepata kura 98,763 sawa na asilimia 0.65, Mgombea wa ADC CHIEF LUTALOSA YEMBA amepata kura 66,049 sawa na asilimia 0.43, Mgombea HASHIM RUNGWE SPUNDA wa Chama Cha CHAUMMA amepata kura 49,256 sawa na asilimia0.32.

Mgombea KAMBALA JANKEN MALIK wa NRA amepata kura 8,028 sawa na asilimia 0.05, Mgombea LYMO MACMILLIAN wa TLP amepata kura 8,198 sawa na asilimia 0.05 ambapo Mgombea DOVUTWA FAHMI NASORO wa Chama Cha UPDP amepata kura 7,7785 sawa na asilimia 0.05.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu LUBUVA amesema wananchi 23,161,440 waliandikishwa kupiga kura ambapo wananchi 15,589,639 sawa na asilimia 67.31 wamepiga kura.

Jaji Mstaafu LUBUVA amesema kura halali zilikuwa 15,193,862 sawa na asilimia 97.46 huku kura 402248 sawa na asilimia 2.58 zikiwa batili.

Kutangazwa kwa Dokta MAGUFULI kumefuatia uhakiki na majumuisho ya kura zilizotangazwa kutoka majimbo ya uchaguzi 264 nchini kote kabla ya kumtangaza mshindi wa ngazi hiyo ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo mawakala wa vyama SABA vya siasa walisaini hati ya kukubali matokeo hayo ya urais.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuwa hafla ya kukabidhi vyeti vya ushindi kwa washindi itafanyika tar 30/10/2015 Saa NNE Asubuhi katika Ukumbi wa DIAMOND Jijini DSM.
HUU NDIO USHAURI WA TUME YA HAKI ZA BINAADAMU  NA UTAWALA BORA KWA ZEC

HUU NDIO USHAURI WA TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA KWA ZEC


Pichani ni Mwenyekiti wa Tume ya haki za binaadamu na utawala bora Ndugu Tom Nyanduga akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
Image result for ushauri wa tume ya haki za binadamu kwa zec


Wednesday, January 28, 2015
RAIS KIKWETE AHAMASISHA MCHANGO WA DOLA BILIONI 7.5 KWA AJILI YA CHANJO YA WATOTO NCHI MASIKINI DUNIANI

RAIS KIKWETE AHAMASISHA MCHANGO WA DOLA BILIONI 7.5 KWA AJILI YA CHANJO YA WATOTO NCHI MASIKINI DUNIANI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.…source: GPL
Monday, January 26, 2015
Baraza jipya la Mawazirilatangazwa

Baraza jipya la Mawazirilatangazwa

Dakika chache zilizo pita katibu kiongozi wa Serikali ya Tanzania kwa niaba ya raisi Kikwete ametangaa baraza jipya la mawaziri.
                                          HAYA NI MABADILIKO MAPYA

Wizara ya katiba na sheria ni Dk. Asha Migiro huku aliekuwa naibu akiendelea.
Wizara ya makamo wa raisi nchi na Mungano mabadiliko ni kwa naibu amabae ni ALL MWALIMU

Wizara ya fedha waziri ni SAADA MKUYA na naibu wake wapili ni Adamu Malima na MWIGULU NCHEMBA.
wizara ya viwanda na biashara naibu wake ni Janeth Mmbene.
Wizara ya ulinzi waziri ni Hussen Mwinyi.
Mambo ya Ndani ni MATHIAS CHIKAWE.

Wizara ya Afya waziri ni SEIF RASHID naibu wake ni STEVEN KEBWE.
Wizara ya elimu naibu waziri ni JENISTA MUHAGAMA.
Wizara ya maendeleo ya jamii na watoto PINDI CHAMA.
Wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi waziri ni TAITASI KAMANI na naibu ni KAIKA SALIGIGO PELELE mbunge wa Ngorongoro

Wizara ya Ardhi naibu wake waziri ni JOJI SIMBA CHAWENE.
Wizara ya Maji naibu waziri ni AMOSI MAKALA.
Wizara ya Kilimo naibu waziri ni Godfrey MZAMBI.
Wizara ya Habari utamaduni na michezo naibu wazri ni JUMA NKAMIA.

Wizara ya Mali asili na Utali waziri ni LAZARO NYALANDU naibu wake ni MAHAMAD MGIMWA
Wizara ya nishati naibu waziri ni CHARZI KITANGWA.
WIZARA AU NAFASSI AMBAZO HAZIJATAJWA ZIMESALIA BILA MABADILIKO MFANO WAZIRI WA ELIMU BADO NI SHUKURU KAWAMBO
Ukawa kuhamasisha wananchi wasipige kura ya maoni Katiba mpya

Ukawa kuhamasisha wananchi wasipige kura ya maoni Katiba mpya

 
Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimetangaza rasmi kutoshiriki katika mchakato wa kura ya maoni ya katiba na kwamba kuanzia sasa vitahamasisha wananchi kuunga mkono.

Uamuzi huo umetolewa leo na wenyeviti wa vyama wanaounda umoja huo wa ukawa ambao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa NLD, Makaidi.

Akizungumza wakati wa kutoa msimamo huo Profesa Lipumba amesema wamefikia uamuzi wa kutoshiriki katika zoezi hilo kwa sababu mchakato mzima haukuwa na maridhiano ya kitaifa.

“Vyama vya siasa ikiwemo CCM vilikubaliana mwaka jana kwamba zoezi la kura za maoni lifanyike mwaka 2016 baada ya uchaguzi mkuu, tulisaini wote na Rais Jakaya Kikwete alikubali, kwa nini mabadiliko yafanyike ghafla” amehoji Profesa Lipumba.

Amesema jambo la kushangaza, Rais Kikwete aligeuka na kutangaza kwamba Aprili 30, mwaka huu kuwa siku ya kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya.

Amesema pamoja na kutangaza siku ya kupiga kura, bado uandikishaji katika daftari la wapiga kura haujaanza kwa sababu wanasubiri vifaa.

“Hadi sasa vifaa vya Biometric Voter Registration (BVR) vilivyopo ni seti 250 wakati vinavyohitajika ni seti 7500, tume inasubiri hadi sasa, zoezi hili litafanyika kweli?,” alihoji Lipumba.

“Mbinu hiyo inafanywa na Serikali kwa sababu Wazanzibari ndiyo wanaona kikwazo kwao,” alisema Makaidi.
 
Aprili 16 mwaka jana, Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba kutoka vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD walitoka nje wakidai bunge hilo lilikuwa halijadili maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Back To Top