Breaking News
Loading...

Advert

MICHEZO

MICHEZO

BURUDANI

BURUDANI

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

SIASA & JAMII KWA UJUMLA

Recent Post

Thursday, October 29, 2015
WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WAKISHANGILIA USHINDI KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA DAR ES SALAAM

WANACHAMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WAKISHANGILIA USHINDI KATIKA VIUNGA VYA JIJI LA DAR ES SALAAM


DR. JOHN POMBE MAGUFULI NDIYE RAIS MTEULE WA AWAMU YA 5 TANZANIA

DR. JOHN POMBE MAGUFULI NDIYE RAIS MTEULE WA AWAMU YA 5 TANZANIA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi -NEC imemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi - CCM, Dokta JOHN POMBE MAGUFULI kuwa mshindi wa Urais kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi  NEC Jaji mstaafu DAMIAN LUBUVA amemtangaza Dokta MAGUFULI kuwa amepata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46 akifuatiwa na Mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA aliyepata kura 6,072,848 sawa na asilimia 39.97.

Mgombea ANNA ELISHA MGHWIRA wa Chama Cha ACT WAZALENDO amepata kura 98,763 sawa na asilimia 0.65, Mgombea wa ADC CHIEF LUTALOSA YEMBA amepata kura 66,049 sawa na asilimia 0.43, Mgombea HASHIM RUNGWE SPUNDA wa Chama Cha CHAUMMA amepata kura 49,256 sawa na asilimia0.32.

Mgombea KAMBALA JANKEN MALIK wa NRA amepata kura 8,028 sawa na asilimia 0.05, Mgombea LYMO MACMILLIAN wa TLP amepata kura 8,198 sawa na asilimia 0.05 ambapo Mgombea DOVUTWA FAHMI NASORO wa Chama Cha UPDP amepata kura 7,7785 sawa na asilimia 0.05.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu LUBUVA amesema wananchi 23,161,440 waliandikishwa kupiga kura ambapo wananchi 15,589,639 sawa na asilimia 67.31 wamepiga kura.

Jaji Mstaafu LUBUVA amesema kura halali zilikuwa 15,193,862 sawa na asilimia 97.46 huku kura 402248 sawa na asilimia 2.58 zikiwa batili.

Kutangazwa kwa Dokta MAGUFULI kumefuatia uhakiki na majumuisho ya kura zilizotangazwa kutoka majimbo ya uchaguzi 264 nchini kote kabla ya kumtangaza mshindi wa ngazi hiyo ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo mawakala wa vyama SABA vya siasa walisaini hati ya kukubali matokeo hayo ya urais.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuwa hafla ya kukabidhi vyeti vya ushindi kwa washindi itafanyika tar 30/10/2015 Saa NNE Asubuhi katika Ukumbi wa DIAMOND Jijini DSM.
HUU NDIO USHAURI WA TUME YA HAKI ZA BINAADAMU  NA UTAWALA BORA KWA ZEC

HUU NDIO USHAURI WA TUME YA HAKI ZA BINAADAMU NA UTAWALA BORA KWA ZEC


Pichani ni Mwenyekiti wa Tume ya haki za binaadamu na utawala bora Ndugu Tom Nyanduga akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam
Image result for ushauri wa tume ya haki za binadamu kwa zec


Back To Top