Breaking News
Loading...

Advert

Thursday, March 3, 2016

Baada ya arsenal kufungwa mabao 2 na swanse city.Wenger asema yafutayo.soma zaid.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger ana
wasiwasi kuhusu matokeo ya timu yake na
anasema wachezaji wake wanafaa kuimarika
baada ya kushindwa 2-1 na kilabu ya Swansea.
Mauricio Pochettino,wakati huohuo amekataa
kulaumu mtu baada ya timu yake ya Tottenham
Hotspur inayopigania kuchukua ligi msimu huu
kupoteza kwa West Ham 1-0.
Na mkufunzi wa Manchester City Manuel
Pellegrini amesema kuwa hafikirii kushinda taji la
ligi ya Uingereza baada ya timu yake kucharazwa
3-0 na Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Hiyo inamaanisha kwamba Leicester itasalia
kileleni mwa ligi huku ikiwa kumesalia mechi 10
pekee.
Leicester ina pointi 57, na hivyobasi wameongeza
uongozi wao katika jedwali la ligi hiyo baada ya
sare ya 2-2 dhidi ya West Bromwich.
Ushindi huo wa Swansea unamaanisha kwamba
Arsenal imepoteza mara tatu mfululizo kwa mara
ya kwanza tangu mwaka 2010.
Mshirikishe mwenzako Unavyoweza
kumshirikisha mwenzako.chanzo bbc swahili.

0 comments :

Post a Comment

Back To Top