Ban kimoon aeleza wasiwasi wake kuhusu uchaguzi jamhuri ya kidemograsia ya kongo.
atibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
ameelezea wasiwasi wake kuhusu hatima ya
uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo, akionya juu ya hatari ya machafuko ya
kisiasa. Taifa hilo linapaswa kuwa na uchaguzi
mkuu mwezi Novemba, lakini nafasi ya kufanyika
kwa uchaguzi huo inazidi kufifia, huku Rais
Joseph Kabila akitiliwa shaka kuwa na mpango
wa kuongeza muhula wake unaomalizika
mwishoni mwa mwaka huu. Akizungumza katika
kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa mjini Newyork kuhusu hali katika ukanda
wa maziwa makuu barani Afrika, Katibu mkuu
Ban alizitaka pande zote zinazohusika kuondoa
tafauti zao kwa njia ya mazungumzo na kuandaa
mazingira ya kufanyika uchaguzi utakaokuwa wa
uwazi, huru na haki kwa kuheshimu katiba.
Alisema ana wasiwasi mkubwa kuhusu
maandalizi ya uchaguzi ujao katika Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo. Ban alilitaka Baraza la
Usalama na viongozi katika eneo hilo kusaidia
kudumisha utulivu wa kisiasa kwa kutafuta njia
ya haraka ya kuitowaJamhuri ya Kidemokrasi ya
Congo katika hali ya hivi sasa.chanzo Dw swahil.
0 comments :
Post a Comment