CUF yatangaza kutoyatambua matokeo ya uchaguzi na kutomtambua Dk.shein kwa ushindi wake soma zaid.
35 PM
Kufuatia ubakaji wa demokrasia kupitia
kile kilichoitwa uchaguzi wa marudio
uliofanywa juzi tarehe 20 Machi, 2016,
jana Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar, Jecha Salim Jecha, alikamilisha
kazi aliyoagizwa kwa kutangaza kile
alichokiita matokeo ya uchaguzi wa Urais.
Chama Cha Wananchi (CUF) kilishaeleza
msimamo wake kuhusu ubakaji huo wa
demokrasia kupitia taarifa yake kiliotoa
tarehe 18 Machi, 2016. Baada ya hatua ya
jana tunaweka msimamo wetu kwamba:
1. Hatutambui hicho kinachoitwa matokeo
ya uchaguzi wa marudio wa tarehe 20
Machi, 2016 na kwa maana hiyo
hatumtambui huyo aliyedaiwa kuwa
mshindi na kwa msingi huo huo
hatutoitambua wala kushirikiana na
Serikali itakayoundwa kutokana na
matokeo hayo batili ya uchaguzi batili.
2. Tunawapongeza kwa dhati Wazanzibari
wote kwa ukomavu wao mkubwa wa
kisiasa waliouonesha kwa kuitikia wito wa
mpendwa wao Maalim Seif Sharif Hamad
na chama chao cha CUF na kutoshiriki
katika uchaguzi huo batili. Kwa ujasiri
wao huo wameudhihirishia ulimwengu
kwa njia za amani na za kistaarabu
kwamba chaguo lao ni Maalim Seif Sharif
Hamad. Kwa mara nyengine tena
Wazanzibari wameyathibitisha maamuzi
yao ya kidemokrasia waliyoyafanya kupitia
uchaguzi huru na wa haki wa tarehe 25
Oktoba, 2015.
3. Tunavipongeza vyombo vya habari vya
ndani na nje na jumuiya ya kimataifa kwa
kuonesha hali halisi ilivyokuwa na jinsi
Wazanzibari walivyoikataa CCM,
walivyowakataa watawala na walivyokataa
kutumika kubaka demokrasia. Wazanzibari
wameandika historia nyengine mbele ya
macho ya ulimwengu. Kwa mara nyengine
tena Wazanzibari wameshinda.
4. Tunajua Wazanzibari wana hamu ya
kujua hatua zinazofuata katika kusimamia
maamuzi yao ya kidemokrasia
waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.
Chama chao kinawatoa wasiwasi
Wazanzibari kwamba hakijayumba na
kinafuatilia haki yao hiyo kwa njia za
amani na za kidemokrasia na kitakuwa
kikiwaeleza kila kinachoendelea.
HAKI SAWA KWA WOTE
NASSOR AHMED MAZRUI
NAIBU KATIBU MKUU – CUF
22 Machi 2016
.chanzo jamii forums.
0 comments :
Post a Comment